Mauaji ya Gaza: Israel yashambulia shule na kuua watoto wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i114862-mauaji_ya_gaza_israel_yashambulia_shule_na_kuua_watoto_wa_palestina
Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimeshambulia kambi mbili za shule katika Ukanda wa Gaza, na kuua Wapalestina wasiopungua 30 waliokimbilia makazi yao.
(last modified 2024-08-05T04:22:58+00:00 )
Aug 05, 2024 04:22 UTC
  • Mauaji ya Gaza: Israel yashambulia shule na kuua watoto wa Palestina

Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimeshambulia kambi mbili za shule katika Ukanda wa Gaza, na kuua Wapalestina wasiopungua 30 waliokimbilia makazi yao.

Mashambulizi ya anga ya utawala huo yalilenga shule za al-Nasr na Hassan Salama katika mji wa Gaza siku ya Jumapili.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Palestina Mahmoud Basal amesema katika taarifa kwamba vikosi vya utawala huo vinafanya "mauaji makubwa" kwa kulipua majengo ya shule ambayo yalikuwa yakihifadhi watu waliokimbia makazi yao Gaza.

Ametaja matukio ya mashambulizi hayo kuwa "mabaya na ya kusikitisha" huku watoto wakiwa asilimia 80 ya waliouawa na kujeruhiwa. Harakati ya Hamas pia imelaani shambulio la mabomu katika shule hizo, ambazo "zilikuwa zimejaa watu waliokimbia makazi yao.

Hamas aidha imesema utawala haramu  wa Israel unafanya mauaji kwa makusudi dhidi ya raia. Israel imeshambulia takriban vituo 172 vya makazi ya watu waliokimbia makazi yao - miongoni mwao shule 152 - tangu jeshi la utawala huo lilipoanzisha vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza mwezi Oktoba.

Taarifa zinesema zaidi ya watu 1,040 wameuawa katika mashambulizi dhidi ya shule, "na mauaji haya ni sehemu ya uhalifu unaoendelea wa Israel dhidi ya watu wetu wa Palestina kwa mwezi wa 10 mfululizo."

Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Palestina imesema Israel na Marekani zinahusika na "mauaji yanayoendelea dhidi ya watu wa Gaza."

Kulingana na takwimu za hivi punde zilizochapishwa na Wizara ya Afya ya Gaza, takriban Wapalestina 39,600 wameuawa hadi sasa katika vita vya Israel dhidi ya Gaza, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.