Wanajeshi magaidi wa Israel walioangamizwa Ghaza wapindukia 700
Televisheni ya utawala wa Kizayuni ilitangaza jana Jumanne kwamba, idadi ya wanajeshi wa dola hilo la kigaidi walioangamizwa kwenye Ukanda wa Ghaza tangu tarehe 7 Oktoba 2023 imeshapindukia 700 kutokana na kuangamizwa wanajeshi wengine kadhaa wa Israel wiki moja iliyopita.
Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, televisheni ya utawala wa Kizayuni iitwayo KAN imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, tangu ulipoanza uvamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza tarehe 7 Oktoba 2023, idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamizwa wameshapindukia 700.
Licha ya kwamba Israel inachuja mno habari, lakini jeshi la utawala huo dhalimu Jumapili lililazimika kutangaza kuangamizwa mmoja wa afisa wa ngazi za juu wa jeshi lake kutoka brigedi ya 9207 na kukiri kwamba hadi hivi sasa wanajeshi 702 wa Israel wameshaangamizwa katika vita vya Ghaza. Siku tano nyuma pia, utawala wa Kizayuni ulikiri kuangamizwa wanajeshi wengine kadhaa wa Israel huko Ghaza.
Kanali za televisheni za utawala wa Kizayuni zimekiri pia kwamba kwa uchache maafisa 15 wa ngazi za juu wa jeshi la Israel wameshaangamizwa hadi hivi sasa hasa wale wa kikosi maalumu cha Golan.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliojeruhiwa hadi hivi sasa huko Ghaza ni 4,387, kati yao wanajeshi 2,257 wameangamizwa katika vita vya nchi kavu.
Kama tulivyotangulia kusema, utawala wa Kizayuni wa Israel umeviwekea sheria kali sana vyombo vya habari ili kuvizuia kutangaza ukweli kuhusu vita kati ya Israel na kambi ya Muqawama, lakini hata hizo habari zinazotangazwa baada ya kuchujwa kupindukia zinaonesha hasara kubwa inazopata Israel kila siku.