WHO: Dawa pekee ya kudumu kwa watu wa Gaza ni amani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115806-who_dawa_pekee_ya_kudumu_kwa_watu_wa_gaza_ni_amani
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, suluhisho pekee la ulinzi wa watoto wa Kipalestina ni kupatikana na kudumishwa amani huko katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Aug 30, 2024 03:51 UTC
  • WHO: Dawa pekee ya kudumu kwa watu wa Gaza ni amani

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, suluhisho pekee la ulinzi wa watoto wa Kipalestina ni kupatikana na kudumishwa amani huko katika Ukanda wa Gaza.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema hayo huku chanjo ya umma dhidi ya polio huko Gaza ikitarajiwa kuanza Jumapili (Septemba 1), na kusisitiza kwamba, dawa pekee ya kudumu kwa watu wa Gaza ni amani.

Kuhusiana na hili, Tedros Adhanom ameandika kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa X: Kulingana na mipango, kampeni ya chanjo dhidi ya polio huko Gaza itaanza Septemba 1, na Shirika la Afya Duniani linakaribisha kusimamishwa kwa vita ili kutekeleza kampeni hii.

Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wametoa wito kwa Israel na Hamas kusitisha vita Gaza kwa sababu za kiutu, ili kuruhusu kuanza kwa kampeni ya chanjo ya polio.

 

Takriban miezi 10 ya vita na mashambulizi makali ya utawala katili Israel imesambaratisha huduma ya afya katika Ukanda wa Gaza na kuvuruga mzunguko wa kawaida wa utoaji chanjo kwa watoto, na kuwaacha wakiwa kwenye hatari ya kupata magonjwa mbalimbali yanayoweza kuzuilika ukiwemo ugonjwa hatari wa kupooza, polio. Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha kuwepo kwa wagonjwa wa polio baada ya kufanyiwa uchunguzi sampuli kadhaa za maji taka zilizochukuliwa kutoka Gaza.

 msemaji wa WHO, Christian Lindmeier alisema kuwa usitishaji mapigano utakuwa suluhisho "bora zaidi", kabla ya kutoa wito angalau kwa barabara za eneo hilo kuwekwa wazi na kusaidia upatikanaji salama wa matibabu na vifaa vingine vya msaada viweze kupita.