Hizbullah yaendelea kuiadhibu Israel kwa maroketi na ndege zisizo na rubani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i116060-hizbullah_yaendelea_kuiadhibu_israel_kwa_maroketi_na_ndege_zisizo_na_rubani
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa imetekeleza mashambulizi katika maeneo mengi ya Israel ili kukabiliana na uvamizi wa kikatili dhidi ya Gaza na kulipiza kisasi mashambulizi dhidi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Sep 06, 2024 03:56 UTC
  • Hizbullah yaendelea kuiadhibu Israel kwa maroketi na ndege zisizo na rubani

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa imetekeleza mashambulizi katika maeneo mengi ya Israel ili kukabiliana na uvamizi wa kikatili dhidi ya Gaza na kulipiza kisasi mashambulizi dhidi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon.

Hizbullah ilisema katika taarifa fupi kwamba wapiganaji wake walivurumisha idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani za kamikaze na marokezi BM-21 Grad kwenye kambi ya jeshi katili la Israel ya Ramot Naftali siku ya Alhamisi jioni. Kambi hiyo ya jeshi la Kizayuni ililengwa kwa mafanikio katika operesheni.

Kundi hilo la muqawama pia limetangaza kutumia ndege zisizo na rubani kulenga kituo kikubwa cha kijeshi cha Beit Hillel ambacho kimejengwa hivi majuzi.

Hizbullah imesema mashambulizi hayo yalikuwa ya kuuadhibu utawala haramu wa Israel kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel kwenye miji ya mpakani kusini mwa Lebanon na pia jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Kumekuwepo na mapigano baina ya Hizbullah na utawala haramu wa Israel  tangu mapema mwezi Oktoba mwaka jana, muda mfupi baada ya utawala huo ghasibu kuanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Hizbullah imeapa kuendeleza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi maadamu utawala wa Israel unaendelea na vita vyake vya Gaza. Hadi sasa katika mauaji ya kimbari ya Gaza utawala haramu wa Israel umewaua Wapalestina wasiopungua 40,878 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.