'Fimbo ya Sinwar' yazaa msemo mpya wa Kiarabu kwa ushujaa wa kiongozi huyo wa Palestina
Kitendo cha mwisho cha upinzani alichoonyesha kiongozi wa Hamas Shahidi Yahya Sinwar, kilichonaswa na kamera ya ndege isiyo na rubani ya jeshi la utawala wa Kizayuni na kurushwa hewani duniani kote, kimeibua msemo mpya wa lugha ya Kiarabu wenye maana ya 'ukinzani' na kuashiria moyo usiotetereka wa Wapalestina wa kupambana hadi pumzi ya mwisho.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wameshiriki kutoa maelezo sawa na hayo kuelezea kitendo cha mwisho cha kiongozi huyo wa Hamas na kuufasiri msemo Fimbo ya Sinwar kwa kusema:
Zafarul-Islam Khan, mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Jamii ya Wachache ya Delhi nchini India amesema, "Walidhani amekufa, na pamoja naye, imekufa pia Harakati ya Uhuru wa Palestina. Lakini ndani ya siku chache za kuuawa kwake, Sinwar amekuwa ngano. Methali mpya ya Kiarabu imetungwa hivi punde: "Nilimpiga kwa fimbo ya Sinwar", ikimaanisha, nilipigana naye kwa nguvu zangu zote hadi pumzi ya mwisho".
Mtumiaji mwingine wa mitandao ya kijamii, Tariq Mehmood, amesema, "Fimbo ya Sinwar ina nguvu zaidi kuliko Tembeo ya David, inafyatua kutoka kwenye mioyo ya mamilioni". Tembeo ya David ni mojawapo ya mitambo kadhaa ya ulinzi wa makombora inayotumiwa na Israel.
Wataalamu wa masuala ya usalama wamesema jeshi la utawala wa Kizayuni lilifanya makosa kwa kusambaza video ya lahadha za mwisho za uhai wa Sinwar, kwa sababu imemtengenezea taji kiongozi huyo wa Muqawama wa Palestina.../