Magaidi 2,000 wauawa huko Syria katika operesheni za kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119724-magaidi_2_000_wauawa_huko_syria_katika_operesheni_za_kijeshi
Duru za Syria zinasema kuwa karibu magaidi 2,000 wakufurishaji wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni wameuawa kaskazini mwa nchi hiyo ya Kiarabu katika mashambulio ya pamoja yaliyofanywa na jeshi la Syria kwa kushirikiana na Russia.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Dec 04, 2024 23:39 UTC
  • Magaidi 2,000 wauawa huko Syria katika operesheni za kijeshi

Duru za Syria zinasema kuwa karibu magaidi 2,000 wakufurishaji wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni wameuawa kaskazini mwa nchi hiyo ya Kiarabu katika mashambulio ya pamoja yaliyofanywa na jeshi la Syria kwa kushirikiana na Russia.

Magaidi hao wameuawa katika operesheni za vya hivi punde  za kijeshi ambazo zililenga maeneo ya mikusanyiko ya magaidi.

Hapo awali, iliripotiwa kuwa jeshi la Syria lilianzisha mfululizo wa operesheni zilizofanikiwa kaskazini mwa Hama, na kupanua eneo la usalama kuzunguka mji huo kwa kilomita 20.

Wakati huo huo magaidi wakufurishaji  na vyombo vya habari katika nchi za Magharibi na za kieneo zinazowaunga mkono, wameanzisha kampeni kali ya propaganda kwa madai kuwa magaidi hao wameingia Hama.

Jeshi la Syria na likishirikiana na jeshi la Russia limetekeleza  operesheni kubwa ya kukabiliana na ugaidi, na kusababisha magaidi na wafuasi wao wa Magharibi kuanzisha kampeni kamili ya vyombo vya habari kwa lengo la kuchafua jitihada za majeshi ya Syria dhidi ya ugaidi.