Shambulio la magaidi Halab Syria kwa msaada wa Uturuki na Israel
Qusay Abdul Jabbar al-Dahhak, mwakilishi wa kukdumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kwamba nchi yake imevamiwa na magenge ya kigaidi na kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kwamba kuna mikono ya nje ya kieneo na kimataifa ndiyo inayoyasaidia magenge ya kigaidi kufanya jinai nchini Syria.
Duru mbalimbali zinasema kuwa, mashambulizi ya hivi sasa ya kigaidi nchini Syria yasingewezekana bila ya kushiriki Uturuki na utawala wa Kizayuni na yamefanyika kufuatia mashambulio ya mara kwa mara ya anga ya Israel katika ardhi ya Syria.
Jumatano ya wiki iliyopita Syria ilikumbwa na wimbi jipya la mashambulizi ya magenge ya kigaidi ambayo yaliteka kwa kasi baadhi ya maeneo ya mkoa wa Halab vikiwemo baadhi ya vituo muhimu. Uvamizi huo ulifanyika muda mchache tu baada ya utawala wa Kizayuni kulazimika kusimamisha vita na Hizbullah ya Lebanon kutokana na kipigo kikali ulichokipata kutoka kwa wanamapambano hao wa Kiislamu.
Kasi iliyoonekana kwenye uvamizi wa magenge ya kigaidi nchini Syria iliyopelekea kutekwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Halab; pekee ni ushahidi tosha kwamba magenge hayo ya ukufurishaji yamesaidiwa na madola ya kigeni.
Vilevile, kusaidifiana mashambulizi hayo makubwa ya magenge ya kigaidi nchini Syria na kuanza kutekelezwa makubaliano ya kusimamisha vita baina ya Israel na Lebanon ni ushahidi mwingine unaothibitisha kwamba magenge ya kigaidi Syria yanafanya jinai zao kwa msaada kamili wa kambi ya Kizayuni-Kimarekani na lengo lao hasa ni kutoa pigo kwa kambi ya Muqawama iliyosimama imara kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Huku hayo yakiripotiwa, Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Meja Jenerali Mohammad Baqeri amefanya mazungumzo ya simu kwa nyakati tofauti na waziri mpya wa ulinzi wa Russia, Andrey Removich Belousov pamoja na Mkuu wa Jeshi la Iraq, Jenerali Yarallah na Mkuu wa Jeshi la Syria, Jenerali Abdul Karim na wote amewatahadharisha kuhusu hatari ya mashambulizi mapya ya magenge ya kigaidi huko Syria na kusisitiza kuwa hiyo ni hatua ya awali ya njama mbaya ya madola ya kibeberu dhidi ya usalama wa ukanda huu mzima. Amesema: Kwenda sambamba uvamizi mpya wa magaidi nchini Syria na kuanza utekelezaji wa makubaliano tete ya kusimamisha vita baina ya Israel na Lebanon ni ushahidi wa kuweko njama inayoendeshwa na kambi ya Marekani-Israel kwa shabaha ya kuidhoofisha Syria na kila anayeiunga mkono Palestina. Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa naye amelaani njama za Uturuki na Israel kwenye jinai hizo mya za magaidi na amesisitiza kuwa Damascus itaendelea kusimama kidete kulinda haki ya kujitawala ardhi nzima ya Syria.
Wakati huo huo picha na video zilizosambazwa na magaidi wa Tahrir al Sham (Jabhatun Nusra) walipovamia na kuteka baadhi ya maeneo ya Halab huko Syria zinaonesha wazi kwamba magaidi hao hawafichi tena uungaji mkono wa Uturuki kwao kiasi kwamba hata wamepandisha bendera za Uturuki kwenye nguzo za maeneo waliyoyateka. Zaidi ya hayo, mwakilishi wa Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa anaamini kuwa, utawala wa Kizayuni na Uturuki zimeyapa magenge ya kigaidi misaada isiyo na idadi zikiwemo silaha na zana za kivita, magari ya deraya, ndege zisizo na rubahi na tekmolojia za kisasa ambazo ziliwasaidia magaidi hao kuvamia na kuteka kwa kasi baadhi ya maeneo ya Halab huko Syria.
Abdul Bari Atwan, mchambuzi maarufu wa ulimwengu wa Kiarabu na mhariri wa gazeti la Ray al Yaum ameandika: Mashambulizi ya wapinzani wa serikali ya Syria wakiongozwa na Jabhatun Nusra yamefanyika kwa kushirikiana na wanaejshi wa kigeni. Mashambulizi hayo hayakuwa ya kushitukiza, bali ni njama ambazo zilipangwa kwa miezi kadhaa nyuma na kambi ya Marekani-Israel-Uturuki ili kufifiliza kushindwa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza na Lebanon.