WHO: Mashambulizi Kaskazini mwa Gaza yanakwaza ufikishaji wa huduma za afya
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119850-who_mashambulizi_kaskazini_mwa_gaza_yanakwaza_ufikishaji_wa_huduma_za_afya
Shirika la Afya la Duniani WHO limetangaza kuwa, mashambulizi ya Israel yanayoendelea Kaskazini mwa Gaza yanaendelea kuzuia ufikishaji wa huduma muhimu za afya zinazohitajika sana.
(last modified 2024-12-07T23:00:54+00:00 )
Dec 07, 2024 23:00 UTC
  • WHO: Mashambulizi Kaskazini mwa Gaza yanakwaza ufikishaji wa huduma za afya

Shirika la Afya la Duniani WHO limetangaza kuwa, mashambulizi ya Israel yanayoendelea Kaskazini mwa Gaza yanaendelea kuzuia ufikishaji wa huduma muhimu za afya zinazohitajika sana.

Dkt. Richard Peeperkorn ambaye ni mwakilishi wa WHO katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Palestina  amesema “Ufikiaji wa hospitali za Kamal Adwan, Al Awda na Indonesia bado umewekewa vikwazo vikali, huku kukiripotiwa uhaba mkubwa wa vifaa vya matibabu, mafuta na vitengo vya damu na operesheni za WHO zinaendelea kutatizwa kwa kiasi kikubwa.”

Amesema “tangu Oktoba 2023 na kufikia tarehe 4 Desemba mwaka huu asilimia , 58 ya operesheni 273 zilizopangwa kuongozwa na WHO ndani ya Gaza aidha zilikataliwa, kufutwa au kuzuiwa, hukukukiwa na operesheni chache zaidi zinazokamilika Kaskazini mwa Gaza.”

Baada ya wiki 7 za majaribio bila mafanikio na kukataliwa operesheni za msaada, timu ya kimataifa ya matibabu ya dharura EMT hatimaye ilitumwa katika Hospitali ya Kamal Adwan ili kuisidia hospitali hiyo ifanye kazi  na timu ziilijumuisha madaktari wawili wa upasuaji, wauguzi wawili wa dharura, daktari na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake.