Mazungumo ya Astana kuhusu Syria yafanyika Doha Qatar
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119852-mazungumo_ya_astana_kuhusu_syria_yafanyika_doha_qatar
Kikao cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Uturuki na Russia kilifanyika jana Jumamosi katika mji mkuu wa Qatar Doha katika fremu ya kikao cha mchakato wa Astana kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
(last modified 2024-12-07T23:01:16+00:00 )
Dec 07, 2024 23:01 UTC
  • Mazungumo ya Astana kuhusu Syria yafanyika Doha Qatar

Kikao cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Uturuki na Russia kilifanyika jana Jumamosi katika mji mkuu wa Qatar Doha katika fremu ya kikao cha mchakato wa Astana kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.

Mkutano huo umeitishwa kwa minajili ya kujadili matukio ya hivi karibuni nchini Syria hasa baada ya makundi ya wabeba silaha nchini Syria kuibuka tena nchini humo.

Iran, Russia na Uturuki zikiwa pande tatu zenye kusimamia mchakato wa asatana zimewahi kukutana na kujadiliana katika mikutano ya awali ya Astana na mkutano huu umefanyika Doha, Qatar, kwa kuzingatia hali na mvutano na migogoro ya hivi karibuni nchini Syria.

Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kiigeni wa Iran hapo awali alitangaza kuhusu kufanyika kwa mkutano huu mjini Doha kwamba mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Astana utafanyika kutokana na kuwepo kwa mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Uturuki na Russia huko Doha.

Iran, Uturuki na Russia ni nchi zinazosimamia mchakato wa Astana ambazo zinafanya juhudi ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.