Iran na Qatar zasisitiza kuimarisha uhusiano
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar kwa mara nyingine tena zimesiisitiza azma yao ya kuimarisha na kustawisha zaidi uhusiano wao.
Sisitizo hilo limetolewa katika mazungumzo ya Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, mazungumzo ambayo yamefanyikka katika mji mkuu wa Qatar Doha.
Viongozi hao wawili walijadili uhusiano wa pande mbili, masuala ya kikanda, na matukio ya hivi karibuni nchini Syria.
Araghchi ambaye yuko nchiini Qatar kkwa ajilii ya kushiriki Kongamano la Kimataiifa la Qatar amekutana na kufanya mazungumzo pia pambizoni mwa mkutano huo na Hakan Fidan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki.
Katika mazungumzo yao hayo, Mawaziri wa Mashaurii ya Kigeni wa Iran na Uturuki wamebadilishana mawazo na kujadili kadhia ya sasa ya Syria na matukio ya hivi karibuni nchini humo.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran aliwasili Qatar akitokea Iraq ambapo siku ya Ijumaa alikutana na kufanya mashauriano na mwenzake wa Iraq, Fouad Hossein, kama ambavyo alifanya mazungumzo pia na Waziri Mkuu Mohammad Shia al-Sudani na Rais wa Iraq Abdul Latif Rashid.