Israel yashambulia ardhi ya Syria baada ya wanamgmabo kuteka Damascus
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119886-israel_yashambulia_ardhi_ya_syria_baada_ya_wanamgmabo_kuteka_damascus
Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel wameanzisha mashambulizi katika ardhi ya Syria na kuingia katika mji wa Quneitra kusini magharibi mwa nchi hiyo karibu na Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Uvamizi huo umejiri baada ya makundi ya wanamgambo kuchukua udhibiti wa nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2024-12-08T10:48:31+00:00 )
Dec 08, 2024 10:48 UTC
  • Israel yashambulia ardhi ya Syria baada ya wanamgmabo kuteka Damascus

Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel wameanzisha mashambulizi katika ardhi ya Syria na kuingia katika mji wa Quneitra kusini magharibi mwa nchi hiyo karibu na Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo. Uvamizi huo umejiri baada ya makundi ya wanamgambo kuchukua udhibiti wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Vyombo vya habari vya Israel mapema leo vimeripoti kuwa vifaru vya utawala huo ghasibu vimeingia Quneitra kwenye mpaka wa Golan inayokaliwa kwa mabavu na kuvurumisha makombora katika maeneo yanayoizunguka.

Vyombo vya habari vya utawala huo pia viliripoti habari ya kuingia kwa vifaru vya Israel katika mji wa Khan Arnabeh ulioko kaskazini mashariki mwa Quneitra na kilomita tano kutoka mpaka wa Golan inayokaliwa kwa mabavu.

Quneitra iko ndani ya eneo la kuzuizi lililoanzishwa mwaka 1974 kati ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Israel na Syria, lakini Khan Arnabeh iko nje ya hapo na majeshi ya serikali hayaruhusiwi kuingia.

Vyombo vya habari vya vilithibitisha ripoti za uvamizi huo wa Israel na kusema kuwa hayo yametokea baada ya utawala huo wa Kizayuni kuongeza idadi ya wanajeshi wake katika Golan inayokaliwa kwa mabavu kabla ya kuanguka kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria huko Damascus.