Idadi ya mashahidi Gaza yakaribia watu 45,000
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119896-idadi_ya_mashahidi_gaza_yakaribia_watu_45_000
idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7, 2023) imekaribia watu 45,000.
(last modified 2024-12-08T23:42:03+00:00 )
Dec 08, 2024 23:42 UTC
  • Idadi ya mashahidi Gaza yakaribia watu 45,000

idadi ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7, 2023) imekaribia watu 45,000.

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, hadi sasa Wapalestina 44,708 wameuawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa.

Wizara ya Afya ya Palestina imeongeza kuwa, zaidi ya wafanyakazi 300 wa sekta ya afya, vikosi 35 vya ulinzi wa raia na wafanyakazi 135 wa Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) wameuawa shahidi katika hujuma inayoendelea ya utawala ghasibu wa Israel.

Uungaji mkono wa wazi wa Marekani na nchi za Magharibi umepelekea kushuhudiwa faili jeusi la viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni wanaoua watu wasio na ulinzi wala hatia. Bila shaka wale wote wanaohami na kuunga mkono jinai za Israel wanahusika pia katika jinai na mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.

Takriban wafanyakazi 18 wa vyombo vya habari waliuawa mwezi Novemba katika mashambulizi ya nchi kavu na ya anga ya jeshi katili la Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.