UN: Takriban watu 75 wameuawa Syria katika wiki mbili zilizopita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119998-un_takriban_watu_75_wameuawa_syria_katika_wiki_mbili_zilizopita
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa mamia ya raia wamejeruhiwa huko Syria katika muda wa wiki mbili zilizopita na karibu 75 wameuawa.
(last modified 2024-12-11T03:53:37+00:00 )
Dec 11, 2024 03:53 UTC
  • UN: Takriban watu 75 wameuawa Syria katika wiki mbili zilizopita

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa mamia ya raia wamejeruhiwa huko Syria katika muda wa wiki mbili zilizopita na karibu 75 wameuawa.

Maafisa wa afya wa Syria wameripoti kuwa, raia wasiopungua 75 wakiwemo watoto 28 na wanawake 11 wameuawa katika maeneo ya kaskazini magharibi mwa nchi hiyo pekee tangu kuanza mapigano nchini humo kuanzia Novemba 26 hadi Disemba 8 mwaka huu. 

Aidha raia 282 wamejeruhiwa wakiwemo watoto 106 na wanawake 56. 

OCHA pia imeripoti kuwa hali ya usalama na kibinadamu huko Syria bado inalegalega.

Wapinzani wanaobeba silaha wa Syria tarehe 8 mwezi huu waliingia katika mji mkuu wa nchi hiyo Damascus na kuudhibiti baada ya jeshi la Syria kuondoka mjini humo.

Wapinzani wa Syria wenye silaha 

Baada ya hapo kamandi ya jeshi la Syria ilitoa taarifa na kutangaza kuanguka utawala wa Rais wa nchi hiyo Bashar al Assad.