Hamas: Muqawama katika Ukingo wa Magharibi unaendelea kwa nguvu zote
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120082-hamas_muqawama_katika_ukingo_wa_magharibi_unaendelea_kwa_nguvu_zote
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza kuwa, mashambulizi hayo ya Wazayuni hayawezi kuteteresha imani na irada ya wananchi wa Palestina na kwamba operesheni dhidi ya wavamizi hao zinaendelea.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Dec 13, 2024 03:19 UTC
  • Hamas: Muqawama katika Ukingo wa Magharibi unaendelea kwa nguvu zote

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza kuwa, mashambulizi hayo ya Wazayuni hayawezi kuteteresha imani na irada ya wananchi wa Palestina na kwamba operesheni dhidi ya wavamizi hao zinaendelea.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, harakati ya Hamas imetoa taarifa kukhusu kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kumuua shahidi kijana wa Kipalestina mjini Nablus asubuhi ya jana Alkhamisi ikisema kuwa, utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu na kigaidi maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan uelewe kwamba hauwezi kuvunja imani, irada na mori wa wananchi wa Palestina na Muqawama dhidi ya Israel utaendelea kwa nguvu zote katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Taarifa ya Hamas pia imesema: Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na maeneo yote yanayohusika na Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa yataendeleza mashambulizi yao kwa nguvu zao zote dhidi ya adui Mzayuni, mashambulizi ambayo yatautikisa utawala huo ghasibu na kukwamisha njama zake.

Hivi sasa utawala katili wa Kizayuni mbali na jinai zake za kuchupa mipaka huko Ghaza, unafanya uvamizi wa mara kwa mara wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kiasi kwamba kwa zaidi ya miezi 14 sasa Ukingo wa Magharibi unashuhudia mapambano ya moja kwa moja ya wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina dhidi ya utawala vamizi wa Israel ambao njama yake kuu ni kuuteka ukingo huo na kuunganisha na maeneo mengine ya Wapalestina unayoyakalia kwa mabavu tangu mwaka 1948..