Kutoadhibiwa na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120158-kutoadhibiwa_na_kuendelea_jinai_za_utawala_wa_kizayuni
Richard Burgon, mbunge wa Bunge la Uingereza amekosoa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa, kutoadhibiwa utawala huo katika vta vya Gaza kumezidi kuitia kiburi Tel Aviv.
(last modified 2024-12-14T23:40:16+00:00 )
Dec 14, 2024 23:40 UTC
  • Kutoadhibiwa na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni

Richard Burgon, mbunge wa Bunge la Uingereza amekosoa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria na kusisitiza kuwa, kutoadhibiwa utawala huo katika vta vya Gaza kumezidi kuitia kiburi Tel Aviv.

Utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza ulianzisha vita na mauaji makubwa ya kimbari katika eneo hilo la Palestina Oktoba 7 mwaka jana kwa himaya na misaada ya pande zote ya Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi. Hadi sasa Israel imewauwa shahidi Wapalestina karibuni elfu 50 na kujeruhi karibu 110,000. Utawala wa Israel ulianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Lebanon mwezi Septemba mwaka huu na kuwaua kigaidi makamanda na viongozi wa kisiasa na zaidi ya Walebanoni 4,000.

Hizi si jinai zote na pekee zilizofanywa na utawala wa Kizayuni katika miezi 14 ya karibuni. Utawala huo ghasibu ambao pia umehusika katika kuondolewa madarakani Bashar al Asssd huko Syria umetumia vibaya ukosefu wa amani huko Syria na kushambulia aghalabu ya vituo vya kijeshi na ndege za kivita za nchi hiyo na kukalia kwa mabavu maeneo mengi ya kijiografia ya Syria. Hapokuwa viongozi wa Kizayuni wanafanya kila wawezalo kudhihirisha jinai zao hizo kuwa ni mafanikio na ushindi mkubwa, lakini bila shaka kimya cha jamii ya kimataifa na kushindwa au kutokuwa na uwezo mfumo wa kimataifa kuwaadhibu Wazayuni ni miongoni mwa sababu kuu za kuendelea na kupanuka jinai za Tel Aviv. Kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu duniani mkabala wa jinai za utawala ghasibu wa Israel kimeufanya utawala huo uendelea kuwauwa wanawake na watoto wa Kipalestina na Lebanon na kufanya jinai mpya nchini Syria.

Mauaji ya kimbari ya Israel dhdi ya wanawake na watoto wa Kipalestina 

Ijapokuwa taasisi za kimataifa kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) zimejitahidi kiasi kuanika jinai za Israel hata hivyo maamuzi na hukumu za taasisi hizo hazina dhamana ya utekelezaji. Hivi karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ilitoa hati ya kukamatwa  Benjamin Netanyahu, na Yoav Galant, Waziri wa Vita wa zamani wa utawala wa Israel kwa kosa na kutenda jinai za vita na uhalifu dhidi ya binadamu. Ingawa nchi nyingi duniani zimeunga mkono na kukaribisha hukumu hiyo ya ICC ya kumtia nguvuni Netanyahu na Gallant na kutangaza kuwa ziko tayari kutekeleza agizo hilo, hata hivyo serikali ya Marekani imeendelea kukingia kifua jinai za utawala wa Kizayuni na kutangaza kuwa nchi yoyote itakayowakamata Netanyahu na Gallant itakabiliwa na jibu la Marekani ikiwa ni pamoja na kuwekewa vikwazo.  

Kupatiwa kinga ya kutoshtakiwa na kutoadhibitiwa utawala wa Kizayuni ni sababu nyingine inayoupa kiburi utawala huo kuendeleza jinai zake. Kuhusiana na suala hili, Richard Burgon, mwakilishi wa eneo la Leeds Mashariki, ambaye hivi karibuni aliwasilisha katika Bunge la Uingereza mpango wa kuuwekea vikwazo utawala wa Kizayuni, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba, "Israel inazidi kuota pembe na kuwa na kiburi kikubwa kwa sababu utawala huo hauchukuliwi hatua yoyote kwa jinai zake za kivita za mara kwa mara dhidi ya watu wa Gaza. Kitendo cha wanajeshi wa Israel cha kuingia katika ardhi ya Syria na kwenda mbali zaidi ya Miinuko ya Golan ni mfano wa wazi wa suala hili." Burgon ameongeza kuwa, kuna udharura na ni lazima utawala mtenda jinai wa Israel uwekewe vikwazo ili uheshimu sheria na kanuni za kimataifa."

Mbunge wa Leeds Mashariki, Richard Burgon 

Kazem Gharib-Abadi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa  hati tu ya kukamatwa  Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, na Yoav Galant waziri wa zamani wa vita wa utawala huo, ambayo ni hatua ya kwanza kabisa ya taasisi ya mahakama. Gharib Abadi ameshiria jinai kubwa za Israel katika Ukanda wa Gaza, Lebanon na kwengineko na kusema: Bado hatuoni mahakama yoyote ya uadilifu ya kufuatilia uhalifu wa utawala wa Kizayuni na viongozi wa watenda jinai wa utawala huo.

Kazem Gharib-Abadi