Idadi ya waliouawa shahidi Gaza yakaribia watu 46,000
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i120326-idadi_ya_waliouawa_shahidi_gaza_yakaribia_watu_46_000
Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7, 2023) imekaribia watu 46,000.
(last modified 2026-05-19T09:45:50+00:00 )
Dec 18, 2024 23:41 UTC
  • Idadi ya waliouawa shahidi Gaza yakaribia watu 46,000

Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu kuanza hujuma kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7, 2023) imekaribia watu 46,000.

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, hadi sasa Wapalestina 45,097 wameuawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa.

Pia shirika hilo la matibabu la Palestina limesema kuwa, jumla ya watu waliojeruhiwa kutokana na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita katika ukanda huo imefikia watu 107,244.

Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza kuwa, zaidi ya wafanyakazi 300 wa sekta ya afya, 35 wa vikosi vya ulinzi wa raia na wafanyakazi 135 wa Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) wameuawa shahidi katika hujuma inayoendelea ya utawala ghasibu wa Israel.

Uungaji mkono wa wazi wa Marekani na nchi za Magharibi umepelekea kushuhudiwa faili jeusi la viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni wanaoua watu wasio na ulinzi wala hatia. Bila shaka wale wote wanaohami na kuunga mkono jinai za Israel wanahusika pia katika jinai na mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.