Aug 14, 2016 07:01 UTC
  • Nasrullah: Makundi kigaidi yanatumikia maslahi ya Marekani

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameyataka makundi ya kigaidi na kitakfiri kuweka chini silaha na yatambue kuwa harakati zao hazina maslahi kwa yeyote isipokuwa adui Marekani.

Akizungumza hapo jana kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 10 wa ushindi wa Hizbullah katika vita vya siku 33 dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, Sayyid Hassan Nasrullah amesema makundi ya kigaidi kama Daesh yanapaswa kuzinduka na kutambua yanapigana kwa niaba ya nani.

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah

Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa, matamshi yanayotolewa na watawala wa Marekani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu yanafaa kutathminiwa kwa karibu na kwa uzito. Amesema kauli kama iliyotolewa hivi karibuni na Donald Trump, mgombea wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican inafaa kuwa tanbihi kwa makundi ya kigaidi na kwa dunia nzima kwa ujumla.

Rais Barack Obama wa Marekani, akitafakari jinsi ya kuwasaidia magaidi wa Daesh

Trump majuzi alisema kuwa kundi la ISIS/Daesh lilibuniwa na Rais Barack Obama wa Marekani kwa ushirikiano wa karibu na Hillary Clinton, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye kwa sasa anagombea kiti cha urais kwa tiketi ya Democrats.

Tarehe 12 Julai mwaka 2006 jeshi la Israel lilishambulia ardhi ya Lebanon kwa muda wa siku 33 na halikufanikiwa kufikia hata lengo moja katika mashambulizi hayo kutokana na mapambano ya kishujaa ya wanamuqawama wa Hizbullah. Wananchi 1,200 wa Lebanon aghalabu yao wakiwa raia wa kawaida waliuawa huku Wazayuni 160 akthari yao wakiwa ni askari vamizi wa utawala ghasibu wa Israel wakiangamizwa katika vita hivyo. 

Tags