Mwandishi wa Kiyahudi Mpinga Uzayuni: Netanyahu ni saratani
-
Benjamin Netanyahu
Alon Mizrahi, mwandishi wa habari wa Kiyahudi anayepinga Uzayuni, ameandika katika ujumbe wake ulioashiria taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu uvimbe wa saratani wa Benjamin Netanyahu kwamba: “Je, saratani yenyewe inaweza kuwa na saratani?”
Mwandishi huyo wa Kiyahudi mpinga Uzayuni ameandika katika akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii wa X:
“Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel ana saratani. Inashangaza – je, saratani yenyewe inaweza kuwa na saratani?”
Ameongeza: “Natumai aendelee kuishi ili acheze katika nafasi yake kwenye onyesho hili la kiendawazimu na la kifo – yaani kumaliza Uzayuni na Israel. Baada ya hapo, anaweza kuondoka na kwenda motoni milele.”
Ofisi ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni jana Ijumaa ilitoa ripoti kuhusu hali ya kiafya ya Benjamin Netanyahu. Iliripotiwa kwamba miezi michache iliyopita alifanyiwa upasuaji na matibabu ya mionzi ili kuondoa uvimbe wa saratani kwenye tezi dume yake.