Sep 26, 2016 14:17 UTC
  • Maulamaa wa Bahrain watoa taarifa ya kumuunga mkono Sheikh Issa Qassim

Maulamaa wa Bahrain leo wametoa taarifa yao katika siku ya kumi ya kukusanyika raia wa nchi hiyo mbele ya nyumba ya mwanazuoni huyo wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.

Taarifa ya maulamaa wa Bahrain imewatolea wito watu wote waliokusanyika kumuunga mkono Sheikh Issa Qassim kuendelea hatua hizo. Maulamaa wa Bahrain wameutaja uungaji mkono wa wananchi kwa Sheikh Issa Qaasim kuwa ni kusimama kidete kwa raia hao mbele ya siasa za dhulma za utawala wa Aal Khalifa;  na kueleza kuwa wanataraji kwamba hatua hizo zitaathiri siasa za kiwendawazimu za utawala wa Bahrain.

Wananchi wakiandamana kumuunga mkono Sheikh Issa Qassim

Mwezi Juni mwaka huu utawala wa Bahrain ulimfutia uraia Sheikh Issa Qaasim mwanazuoni wa Kishia wa nchini humo; kitendo kilichokabailiwa na radiamali kali miongoni mwa Waislamu wa Kishia wa Bahrain na ulimwenguni kwa ujumla. Wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano ya amani dhidi ya serikali tangu mwezi Februari mwaka 2011. 

Tags