Makumi wauawa na kujeruhiwa katika hujuma Aleppo Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16447-makumi_wauawa_na_kujeruhiwa_katika_hujuma_aleppo_syria
Habari kutoka Syria zinasema kwa akali watu 18 wameuwa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika hujuma ya maroketi iliyotekelezwa na makundi ya kitakfiri katika eneo la makazi ya watu mjini Aleppo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Oct 01, 2016 04:42 UTC
  • Makumi wauawa na kujeruhiwa katika hujuma Aleppo Syria

Habari kutoka Syria zinasema kwa akali watu 18 wameuwa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika hujuma ya maroketi iliyotekelezwa na makundi ya kitakfiri katika eneo la makazi ya watu mjini Aleppo.

Habari zinasema kuwa, zaidi ya watu 60 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo la jana Ijumaa lililolenga wilaya za Midan, Azizia na Villat katika mji huo wa kaskazini mwa Syria.

Duru za hospitali zinasema kuwa yumkini idadi ya waliouawa katika hujuma hiyo ikaongezeka kutokana na majeraha mabaya waliyoyapata wahanga wa shambulizi hilo.

Athari za hujuma ya Aleppo

Jeshi la Syria likisaidiwa na vikosi vya jeshi la anga la Russia hivi karibuni lilianzisha oparesheni kubwa ya kijeshi kwa minajili ya kuwatimua magaidi katika mji wa Aleppo na hadi sasa magaidi wa Daesh  na wa makundi mengine ya kigaidi zaidi ya 1000 wameuliwa na wengine karibu 2500 kujeruhiwa.