Apr 29, 2017 07:43 UTC
  • Utawala wa Bahrain waendelea kuzuia Sala ya Ijumaa eneo la Diraz

Askari wa utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain, kwa mwezi wa 10 mfululizo wamezuia Sala ya Ijumaa kusaliwa katika eneo la Diraz nchini humo.

Taarifa zinasema wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa jana waliwazuia waumini kuingia latika eneo lililozingirwa la Diraz na kuzuia Sala ya Ijumaa na kwa msingi huo waliokuwa wamefika eneo hilo hawakuwa na budi ila kuswali furada katika msikiti wa Imam Sadiq AS.

Tokea mwezi Juni mwaka 2016,  utawala wa Bahrain umekuwa ukizuia sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Sadeq AS katika eneo la Diraz.

Askari wa Bahrain wakiwa wamefunga njia kuzuia Sala ya Ijumaa

Wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga kuvuliwa uraia Sheikh Isa Qassim kwa tuhuma zisizo na msingi kuwa eti anachochea malumbano ya kimadhehebu na ghasia licha ya kuwa mwanachuoni huyo ni mashuhuri kwa misimamo yake ya kutetea Umoja wa Kiislamu na maandamano ya amani Bahrain.

Malalamiko na maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya watawala dhalimu wa nchi hiyo yamekuwa yakiendelea tokea tarehe 14 Februrai 2011. Tokea mwanzoni mwa maandamano hayo watawala wa ukoo wa Aal Khalifa wamekuwa wakitekeleza mbinu tofauti za kupambana na wapinzani.

Tags