Jeshi la Iraq linaendeleza jitihada za kuwamaliza Madaesh 100 waliosalia Mosul
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31384-jeshi_la_iraq_linaendeleza_jitihada_za_kuwamaliza_madaesh_100_waliosalia_mosul
Rupoti kutoka Iraq zinasema kuwa, wapiganaji wasiozidi mia moja wa kundi la kigaidi la Daesh ndio waliobakia katika eneo la kale la Mosul.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 05, 2017 23:36 UTC
  • Jeshi la Iraq linaendeleza jitihada za kuwamaliza Madaesh 100 waliosalia Mosul

Rupoti kutoka Iraq zinasema kuwa, wapiganaji wasiozidi mia moja wa kundi la kigaidi la Daesh ndio waliobakia katika eneo la kale la Mosul.

Ripoti zinasema kuwa, jeshi la Iraq limezidisha jitihada za kuhakikisha linawamaliza makumi ya wapiganaji wa kundi ya kiwahabi la Daesh katika eneo la kale la Mosul na kulisafisha kabisa eneo hilo. 

Ripoti hiyo imetolewa baada ya Jeshi la Polisi la Iraq kuangamiza zaidi ya magaidi 60 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika operesheni ya kusafishwa eneo la kale la mji wa Mosul, kaskazini mwa nchi hiyo.

Mzoga wa kamanda mmoja wa kundi la kigaidi la Daesh, Mosul

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iraq, Meja Jenerali Shaker Jodat, amesema kuwa, vikosi vya jeshi la ulinzi la nchi hiyo vinaendeleza operesheni ya kuyasafisha maeneo yaliyobakia na eneo la kale la mji wa Mosul na kuwaokoa wananchi na raia wa kawaida waliokuwa wamezingirwa kwenye mazingira magumu sana na magaidi wa Daesh.

Vikosi vya Jeshi la Iraq Alhamisi iliyopita viliingia katika Msikiti wa al Nuri uliokuwa ukitumiwa na kiongozi wa kundi la Daesh magharibi mwa Mosul, hatua ambayo imehitimisha rasmi dola bandia la "khilafa la mawahabi wa Daesh katika mji huo.