Mfalme wa Bahrain ataka nchi za Kiarabu ziache kususia Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i34529-mfalme_wa_bahrain_ataka_nchi_za_kiarabu_ziache_kususia_israel
Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain amezitaka nchi za Kiarabu kuacha kuusussia utawala haramu wa Israeli.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Sep 18, 2017 09:35 UTC
  • Mfalme wa Bahrain ataka  nchi za Kiarabu ziache kususia Israel

Mfalme Hamad bin Isa Aal Khalifa wa Bahrain amezitaka nchi za Kiarabu kuacha kuusussia utawala haramu wa Israeli.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kizayuni, tamko hilo la Mfalme Hamad liko katika ujumbe wake maalumu kwa kikao cha kundi linalounga mkono lsrael la Simon Wiesenthal Centre mjini Los Angeles Marekani. Aidha matawala huyo wa Bahrain ametaka kuanzishwe uhusiano kamili wa kidiplomasia baina ya Waarabu na Israel.

Tamko hilo linakuja wiki kadhaa tu baada ya Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahju kuutaja uhusiano wa utawala huo na nchi za Kiarabu kuwa mzuri zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule.

Aidha wiki iliyopita kulifichuka ripoti ya mkutano wa viongozi wa ngazi za juu wa utawala wa kifalme wa Saudia na maafisa wa Israel mjini Tel Aviv. Mwezi Juni pia email zilizovuja za balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE nchini Marekani Yousef al Otaiba zilibaini kuwa UAE ina uhusiano wa siri na shirika moja linalounga mkono Israel linalojulikana kama Foundation for Defense of Democracies.

Msikiti wa al Aqsa unaokaliwa kwa mabavu na Israel

Nchi za Kiarabu zinaharakisha kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel wakati ambao utawala huo haramu unaendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina hasa kibla cha tatu cha Waislamu yaani Msikiti wa Al Aqsa.