May 06, 2018 07:29 UTC
  • HRW: Maelfu wanazuiliwa kwa muda mrefu Saudia bila kufunguliwa mashitaka

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekosoa ukiujaki wa haki za binadamu unaofanywa nchini Saudi Arabia na haswa hatua ya utawala wa Aal-Saud ya kuwazuilia kwa vipindi virefu watuhuma wa makosa mbalimbali pasina kuwafungulia mashitaka.

Ripoti ya HRW iliyotolewa leo Jumapili kwa kunukuu takwimu rasmi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imeonyesha kuwa, serikali ya Riyadh imewazulia watu 2,305 kwa zaidi ya miezi sita, wengine hata zaidi ya miaka kumi, pasina kupandishwa kizimbani.

 Sarah Leah Whitson, Mkurugenzi wa Human Rights Watch katika eneo la Mashariki ya Kati amesema, "Iwapo watawala wa Saudi Arabia wanaweza kumzuilia mshukiwa kwa miezi na miezi bila mashitaka yoyote, ni wazi kuwa mfumo wa sheria wa Saudia umevunjika na sio wa kiuadilifu, na la kushangaza hali hii inazidi kuwa mbaya kila uchao."

Katika miezi ya hivi karibuni wanawafalme wapinzani, wakosoaji, wanaharakati wa kisiasa na waandishi wa habari wametiwa mbaroni kwa amri ya Muhammad bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia. 

Saudia pia imekuwa ikitajwa kama moja ya nchi zinazonyonga watu zaidi duniani

Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa, kuna wafungwa wa kisiasa wapatao 30,000 katika magereza ya Saudia, takwimu ambazo zinaakisi kushadidi siasa za kipolisi za utawala wa kidikteta wa Aal Saud dhidi ya wananchi wa nchi hiyo.

Hivi karibuni pia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilikosoa vikali hali ya haki za binadamu nchini Suaudi Arabia na kuitaka serikali ya Riyadh kukomesha hali hiyo.

Tags