Sayyid Hassan Nasrullah: Mashambulizi ya Israel nchini Syria hayavumiliki tena
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48255-sayyid_hassan_nasrullah_mashambulizi_ya_israel_nchini_syria_hayavumiliki_tena
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Syria hayavumiliki tena na inabidi yakomeshwe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 19, 2018 23:22 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrullah: Mashambulizi ya Israel nchini Syria hayavumiliki tena

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Syria hayavumiliki tena na inabidi yakomeshwe.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo usiku wa kuamkia leo kwa mnasaba wa mwezi kumi Muharram, (usiku wa Ashura) na kusisitiza kuwa, kambi ya muqawama inapaswa kutafakari njia za kukomesha mashambulio ya mara kwa mara ya Wazayuni nchini Syria.

Amesema, mashambulizi ya Israel huko Syria yana mfungamano wa moja kwa moja na kushindwa njama za Marekani - Saudia - Israel; na ndio maana hivi sasa utawala wa Kizayuni unafanya njama za kila namna za kuizuia Syria kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa makombora.

Hii ni miongoni mwa jinai kubwa zilizofanywa na magaidi wa ISIS kwa uungaji mkono wa mabeberu wa dunia

 

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, wanajeshi wa Hizbullah wataendelea kuweko Syria hadi pale uongozi wa nchi hiyo utakaposema kuwa hakuna haja tena ya kuweko wanajeshi hao nchini humo.

Amma kuhusu kuendelea kuweko genge la kigaidi la Daesh (ISIS) huko nchini Syria, Sayyid Hassan Nasrullah amesema, Marekani ndiyo inayorefusha uwepo wa baadhi ya mabaki ya magaidi wa Daesh katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mashariki mwa Syria na kwamba hivi sasa magaidi wa ISIS wanahamishiwa Afghanistan, Pakistan, Misri na Yemen baada ya kusambaratishwa huko Iraq na Syria.

Aidha amewakosoa vikali baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu na kusema kuwa, viongozi hasa wa baadhi ya nchi za Kiarabu hivi sasa ni mabalozi wa Marekani na ndio waamuzi wakuu wa mambo yanayofanywa na nchi hizo.