Wairaqi wafanya maandamano Baghdad kuunga mkono matamshi ya Ayatullah Sistani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57696-wairaqi_wafanya_maandamano_baghdad_kuunga_mkono_matamshi_ya_ayatullah_sistani
Wakazi wa mji mkuu wa Iraq, Baghdad wamefanya maandamano makubwa mapema leo chini ya kaulimbiu ya "Timua Waharibifu" wakitangaza uungaji mkono wao kwa kiongozi mkuu wa kidini nchini humo Ayatullah Ali Sistani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 05, 2019 11:57 UTC
  • Wairaqi wafanya maandamano Baghdad kuunga mkono matamshi ya Ayatullah Sistani

Wakazi wa mji mkuu wa Iraq, Baghdad wamefanya maandamano makubwa mapema leo chini ya kaulimbiu ya "Timua Waharibifu" wakitangaza uungaji mkono wao kwa kiongozi mkuu wa kidini nchini humo Ayatullah Ali Sistani.

Ripoti zinasema kuwa, Waandamanaji hao walikusanyika katika barabara kuu ya Palestina na kuelekea Medani ya Uhuru huku wakipiga nara za kuwatimulia mbali waharibifu wanaozusha machafuko na fujo baada ya kuparamia maandamano ya amani ya wananchi wa Iraq. 

Maandamano hayo yamefanyika kuitikia wito uliotolewa na Ayatullah Ali Sistan aliyewaagiza Wairaqi kutambua vibara waliopenyeza kwenye safu za wananchi katika maandamano yao na kuwatimulia mbali. 

Wiki iliyopita maafisa wa serikali ya Iraq waliripoti kuwa, baadhi ya wafanyafujo na watu waliokuwa wameva maski wameingia katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala na kufanya ghasia na fujo kwa kushambulia maeneo ya kidini na vituo vya kidiplomasia kama ubalozi mdogo wa Iran katika mji wa Najaf. 

Maandamano ya Wairaqi, Baghdad

Itakumbukwa kuwa jengo la ubalozi mdogo wa Iran katika mji mtakatifu wa Najaf limechomwa moto na kundi la wahalifu waliokuwa wamevalia maski na duru mbalimbali zinasema watu hao hawakuwa wakazi wa mji huo.

Katika wiki za karibuni baadhi ya miji ya Iraq imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali ngumu ya maisha, huduma mbovu kwa umma, ukosefu wa ajira na ufisadi. Hata hivyo maandamano hayo yameparamiwa na vibara wa nchi za kigeni na hivyo kuibua machafuko. 

Waziri Mkuu wa Iraq Adil Abdul-Mahdi ametangza kuwa ameamua kujiuzulu kutokana na hali iliyopo na ili kuepusha machafuko zaidi nchini humo. Vilevile amelitaka Bunge lichukue uamuzi kuhusiana na kuundwa serikali mpya.