15 Septemba, siku ya ghadhabu ya Waarabu dhidi ya watawala vibaraka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63443-15_septemba_siku_ya_ghadhabu_ya_waarabu_dhidi_ya_watawala_vibaraka
Imarati na Bahrain leo Jumanne zinatarajiwa kutia saini mapatano ya amani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ikulu ya Rais wa Marekani, White House, mjini Washington. Hatua hii imeyakasirisha sana mataifa ya Waislamu na Waarabu ambayo yameitaja kuwa ni usaliti dhidi ya Uislamu, Palestina na Quds tukufu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 15, 2020 15:12 UTC
  • 15 Septemba, siku ya ghadhabu ya Waarabu dhidi ya watawala vibaraka

Imarati na Bahrain leo Jumanne zinatarajiwa kutia saini mapatano ya amani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ikulu ya Rais wa Marekani, White House, mjini Washington. Hatua hii imeyakasirisha sana mataifa ya Waislamu na Waarabu ambayo yameitaja kuwa ni usaliti dhidi ya Uislamu, Palestina na Quds tukufu.

Mapatano hayo yalitazamiwa kusainiwa na mawaziri wa mambo ya nje wa Imarati,Bahrain na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. 

Kuhusiana na kadhia hiyo Waziri Mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh amesema: "Leo Jumanne ni siku nyeusi katika historia ya uliwengu wa Kiarabu na siku ya kufeli Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League). Jumuiya hii sasa ni taasisi ya kuzusha migawanyiko na si jumuiya ya Waarabu. Hii itakuwa tarehe nyingine ya kuongezea katika kalenda ya matukio chungu ya Palestina."

Malalamiko na upinzani dhidi ya hatua hiyo ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano na utawala katili unaoendelea kuua Wapalestina havikuishia katika ngazi ya wanasiasa wa Palestina bali umepanuka zaidi hadi kwenye makundi na harakati za kupigania ukombozi za Palestina na makundi ya wananchi na watetezi wa haki za binadamu na za kiraia katika nchi mbalimbali za Kiislamu. Harakati za mapambano za Palestina zimeitangaza siku ya leo Jumanne tarehe 15 Septemba kuwa ni Siku ya Ghadhabu dhidi ya usaliti huo na kutangaza kwamba Ijumaa ijayo itakuwa siku ya maombolezo ya kitaifa. 

Umma wa Kiislamu unapinga suala la kuanzisha uhusiano na utawala katili wa Israel

Katika nchi nyingine pia makundi na watu wa matabaka tofauti wameungana na wenzao wa Palestina kupinga usaliti huo wa Imarati na Bahrain kupitia mitandao ya kijamii. Baadhi ya watu wameonyesha hasira zao dhidi ya watawala wa Imarati na Bahrain kwa kuwataja kuwa wametupilia mbali hadhi na utambulisho wao wa Kiarabu huku wengine  wakiifanyia maskhara Saudi Arabia inayounga mkono hatua ya nchi hizo kwa kujinadi kuwa ni kinara wa nchi za Kiarabu. Hii ni kwa sbabu japokuwa Riyadh haijatangaza waziwazi uhusiano wake na utawala haramu wa Israel lakini ina uhusiano mkubwa wa siri na utawala huo na tayari imeiruhusu Israel kutumia anga ya nchi hiyo. 

Hasira za Waislamu na Waarabu dhidi ya jinai ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel zinatoa ujumbe kadhaa:

Kwanza ni kwamba tawala za Imarati, Bahrain na Saudi Arabia hazina uungaji mkono wa wananchi. Mhadhiri wa sayansi ya siasa na mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha cha Lahore nchini Pakistan, Farooq Hassanat ameandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter kwamba: "Wanamfalme wa Kiarabu wanajali zaidi anasa na mavazi ya kifakhari badala ya kuwa na wasiwasi kuhusu hali ya watu wanaodhulumiwa wa Palestina. Mahusiano maovu ya watawala hao na utawala haramu wa Israel yanaanika na kuweka wazi shakhsia na dhati zao; hivyo mapatano ya sasa yanaweza kuwa fimbo dhidi ya watawala hao katika siku zijazo."

Watawala vibara wa Kiarabu wameanzisha uhusiano na Israel

Pili ni kwamba, hadi sasa fikra za waliowengi bado zina nguvu kubwa, kwani kama si kuogopa fikra za Waislamu, basi hii leo pia Saudi Arabia ingekuwa bega kwa bega na Imarati na Bahrain huko White House kutangaza waziwazi uhusiano wake wa siri na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tatu ni kwamba, watu wa Palestina wanaweza kutumia nguvu ya fikra za waliowengi katika nchi za Kiislamu na Kiarabu kwa ajili ya kulaani usaliti wa Imarati na Bahrain. Ni kwa sababu hii pia ndiyo maana wanaharakati wa mitandao ya kijamii wameanzisha kampeni ya kusainiwa hati ya nchi ya Paletina.  

Hati ya nchi ya Palestina inayosambazwa sasa katika mitandao ya kijamii inasisitiza kuwa: "Palestina ni nchi ya Kiarabu inayokaliwa kwa mabavu ambayo ni jukumu letu kuikomboa; na aina yoyote ya kufanya uhusiano na utawala vamizi ni usaliti."

Kampeni hiyo imeanzishwa na wanaharakati wnaopinga hatua yoyote ya kuanzishwa uhusiano baina ya nchi za Kiarabu na utawala haramu wa Israel na katika nchi kama Imarati, Saudi Arabia, Oman na kadhalika.