Umoja wa Mataifa wasisitiza kuhitimishwa uvamizi wa utawala wa Kizayuni Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i63451-umoja_wa_mataifa_wasisitiza_kuhitimishwa_uvamizi_wa_utawala_wa_kizayuni_palestina
Baraza la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio likiutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uhitimishe kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 16, 2020 03:13 UTC
  • Umoja wa Mataifa wasisitiza kuhitimishwa uvamizi wa utawala wa Kizayuni Palestina

Baraza la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio likiutaka utawala wa Kizayuni wa Israel uhitimishe kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.

Azimio hilo lililopigiwa kura za ndio 47, kura tatu za hapana zilizopigwa na Marekani, Australia na Canada na nchi nne hazikupiga kura yaani Brazil, Malawi, Togo na Ukraine miongoni mwa nchi wanachama 54 limezingatia taathira za kiuchumi na kijamii za uvamizi wa Israel kwa maisha ya raia wa Palestina. 

Azimip hilo linaeleza kuwa: Uvamizi na kuzikaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kulikofanywa na Israel ni kizingiti kikubwa kwa juhudi za kupatikana ustawi endelevu, mazingira na anga salama ya kiuchumi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ikiwemo Quds Mashariki na Miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavuhuko Syria. 

Baraza la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa limesema kuwa lina wasiwasi mkubwa kutokana hali mbaya ya kiuchumi na kimaisha ya Wapalestina na kutahadharisha kuhusu ongezeko la idadi ya watu wasio na ajira katika Ukanda wa Ghaza ambapo asilimia 60 ya raia hao ni vijana. Baraza hilo limeutaja mzingiro wa muda mrefu wa utawala wa Kizayuni wa Isrel dhidi ya eneo la Ghaza na vizingiti na vizuizi vikali vya kiuchumi dhidi ya raia wa Palestina wa eneo hilo kuwa ni sababu ya hali hiyo mbaya. 

Mzingiro unavyowatesa raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza  

Azimio hilo lililopasishwa na Umoja wa Mataifa limetaka pia kuondolewa vizuizi vyote walivyowekea raia wa Palestina na kuchukuliwa hatua za haraka ili kupunguza maafa yanayoshuhudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu hususan eneo la Ghaza.