Wazayuni karibu 50 waangamia baada ya kukanyagana katika mjumuiko wa kidini
Wazayuni karibu 50 wameangamia baada ya kukanyagana katika mujumuiko wa kidini uliokuwa umehudhuriwa na makumi ya maelefu ya watu kaskazini mwa Israel.
Kwa mujibu wa taarifa, Wazayuni wengine wamejeruhiwa katika mkanyagano huo uliojiri mapema leo Ijumaa huku taarifa zikisema idadi ya waliofariki ni zaidi ya iliyotangazwa rasmi.
Jeshi la utawala haramu wa Israel limesema limetuma vikosi vya uokoaji na msaada wa matibabu kwenda eneo la tukio. Makumi kwa maelfu ya Wazayuni walikusanyika chini ya mlima Meron kwa sherehe za sikukuu ya Kiyahudi inayomuenzi kiongozi mmoja wa kiroho wa karne ya 2 ambaye amezikwa kwenye eneo hilo.
Wazayuni hao wamejumuika huku kukiwa na hofu ya kuenea virusi vya corona miongoni mwa waliokusanyika hapo.
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amelitaja tukio hulo kuwa 'maafa makubwa'.
Baadhi ya walionusurika katika mkanyagano huo wamesema, watu walianza kuangushana muda mfupi baada ya kuwepo kwa ujumbe wa dharura kuwa huenda kukatokea mlipuko wa bomu.
Picha na mikanda ya vídeo imewaonesha maelfu ya Wazayuni wakiwa pamoja kabla ya kila mmoja kuanza kukimbilia usalama wake.