Wanasoka Waislamu waungana na walimwengu kulaani jinai za Israel huko Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70056-wanasoka_waislamu_waungana_na_walimwengu_kulaani_jinai_za_israel_huko_palestina
Jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Baytul-Muqaddas Palestina zimeendelea kulaaniwa kila kona ya dunia ambapo mara hii wanasoka mashuhuri duniani wamejitokeza na kulaani jinai hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 12, 2021 06:53 UTC
  • Wanasoka Waislamu waungana na walimwengu kulaani jinai za Israel huko Palestina

Jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Baytul-Muqaddas Palestina zimeendelea kulaaniwa kila kona ya dunia ambapo mara hii wanasoka mashuhuri duniani wamejitokeza na kulaani jinai hizo.

Wachezaji mashuhuri wa soka wa Kiarabu na Waislamu wameonyesha kusikitishwa kwao na masaibu yanayowakumbwa Wapalestina wa kitongoji cha Sheikh Jarrah na kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi hao madhulumu. Riyadh Mahrez, mchezaji wa timu ya soka ya Manchester City ya Uingereza ambaye ni raia wa Algeria ametuma ujumbe katika mitandao ya kijamii akitangaza kuungana na wananchhi wa Palestina.

Mmoroco Achraf Hakimi anayesakata kabumbu katika timu ya soka ya Inter Milan ya Italia naye ameonyesha kuungana na wananchi wa Palestina. Aidha Mfaransa Paul Pogba aanyechezea klabu ya Manchester United amelaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na kutangaza kuwaunga mkono wananchi hao madhulumu.

Mesut Ozil (katikati) akiwa na wacherzaji wenzake wa Fenerbahce  ya Uturuki

 

Kwa upande wake Mohamed Salah mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool ya Uingereza aambaye ni raia wa Misri ametoa wito kwa viongozi wa duniani kuchukua hatua za kuukomeshha vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji dhidi ya watu wasio na hatia. Sadio Mane mchezaji mwingine wa Liverpool raia wa Senegal ametuma ujumbe katika mtandao wa kijamii wa Instagram unaosema: Free Palestine.

Mesut Ozil, mchezaji wa zamani wa Arsenal anayechezea klabu ya Fenerbahce  ya Uturuki alionekana na wachezaji wenzake wa timu hiyo wakiwa wamevaa tisheti zenye maandishi "Free Palestina", walipokuwa wakifanya mazoeni ya viungo kabla ya mechi yao hapo jana.

Franck Ribey mwanasoka wa Ufaransa na Shkodran Mustafi ambaye kwa sasa anasakata kabumbu nchini Ujerumani baada ya kuondoka Arsenal ya Uingereza ni miongoni wa wanasoka wengine mashuhuri waliotangaza kuwaunga mkono wananchi wa Palestina