Marekani yawawekea vikwazo shakhsia 8 na taasisi 10 za Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i72898-marekani_yawawekea_vikwazo_shakhsia_8_na_taasisi_10_za_syria
Katika kuendelea hatua za uhasama za Washington dhidi ya Syria, jana Wizara ya Fedha ya Marekani iliwawekea vikwazo shakhsia 8 na taasisi 10 za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 29, 2021 03:08 UTC
  • Marekani yawawekea vikwazo shakhsia 8 na taasisi 10 za Syria

Katika kuendelea hatua za uhasama za Washington dhidi ya Syria, jana Wizara ya Fedha ya Marekani iliwawekea vikwazo shakhsia 8 na taasisi 10 za nchi hiyo.

Wizara ya Fedha ya Marekani metoa madai ya kipumbavu na kuwatuhumu shakhsia na taasisi hizo za Syria kuwa wanaunga mkono ugaidi. Majina ya jela 8 za Syria na pia maafisa kadhaa wa usalama wa nchi hiyo yapo katika orodha ya mashirika na taasisi za Syria ambazo zimewekewa vikwazo na Wizara ya Fedha ya Marekani. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria hivi karibuni ililaani vikwazo vya Washington dhidi ya nchi hiyo na kutangaza kuwa ugaidi wa kiuchumi ni aina nyingine ya ugaidi kwa sababu umesababisha kumwagwa damu za wananchi wa Syria na kusambaratisha mafanikio yaliyopatikana kupitia damu za raia hao. Marekani imeiwekea Syria vikwazo vya aina mbalimbali tangu mwaka 2011 ili kuwaunga mkono magaidi nchini humo.   

Zama za Daesh nchini Syria 

Syria ikiwa moja ya nchi wanachama wakuu wa mhimili wa muqawama ina nafasi muhimu katika kukabiliana na njama na mipango haramu ya muungano wa Marekani- Wazayuni na Saudi Arabia.