Az-Zahar: Wazayuni hawana mustakabali wowote Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i77330-az_zahar_wazayuni_hawana_mustakabali_wowote_palestina
Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, mayahudi wazayuni hawana mustakabali wowote katika Palestina na kwamba watu wa ardhi hiyo watawatimua wazayuni hao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 26, 2021 04:15 UTC
  • Az-Zahar: Wazayuni hawana mustakabali wowote Palestina

Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, mayahudi wazayuni hawana mustakabali wowote katika Palestina na kwamba watu wa ardhi hiyo watawatimua wazayuni hao.

Mahmoud Az-Zahar ameliambia shirika la habari la FARS kuwa, vuguvugu la muqawama limeongezeka katika mji wa Baitul Muqaddas na kwamba moja ya madhihirisho muhimu zaidi ya jambo hilo ni operesheni ya "Saiful-Quds" yaani Upanga wa Quds na operesheni ya kufa shahidi ya Fadi Abu Shkhaydam.

Dakta Az-Zahar amezungumzia operesheni hiyo dhidi ya Wazayuni iliyotekelezwa na shahidi Abu Shkhaydam kwa kusema, "operesheni hii inaonyesha ukweli na imani ya watu Waislamu wa Palestina na mapenzi yao makubwa kwa nchi yao; na kila mtu kulingana na uwezo wake anafanya jitihada za kuwatimua mayahudi wazayuni Palestina na hasa katika mji wa Quds, hata kama kujitolea huko kutamalizikia kwa kufa shahidi."

Shahidi Fadi Abu Shkhaydam

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hamas ameongeza kuwa, operesheni hizo zinaendelea na kwamba kama zitasita kwa muda fulani ni kutokana na sababu mbalimbali kama za utayarifu, kuandaa mazingira na kuchagua mahali na wakati mwafaka wa kutoa kipigo angamizi kwa jeshi la kizayuni.

Siku ya Jumapili iliyopita, shahidi Fadi Abu Shkhaydam alitekeleza operesheni ya kujitoa mhanga katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu alipowashambulia na kuwajeruhi wazayuni wanne na kumwangamiza mwingine mmoja na yeye mwenyewe akauawa shahidi.

Katika kumbukumbu ya barua aliyoacha kabla ya kutekeleza operesheni hiyo dhidi ya wazayuni Fadi Abu Shkhaydam ambaye alikuwa mwalimu amesema "nilikuwa na ndoto ya kukutana na Mwenyezi Mungu nikiwa nimekufa shahidi".../