HAMAS: Damu za mashahidi wa Jenin hazitoachwa zimwagike bure
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80924-hamas_damu_za_mashahidi_wa_jenin_hazitoachwa_zimwagike_bure
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, damu za mashahidi wa kambi ya wakimbizi ya Jenin hazitoachwa kumwagika bure na zitalifanya taifa la Palestina lishikamane zaidi ya muqawama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 02, 2022 03:49 UTC
  • HAMAS: Damu za mashahidi wa Jenin hazitoachwa zimwagike bure

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, damu za mashahidi wa kambi ya wakimbizi ya Jenin hazitoachwa kumwagika bure na zitalifanya taifa la Palestina lishikamane zaidi ya muqawama.

Wapalestina wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa Israel kwa siku kadhaa sasa katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na pia kwenye kitongoji cha Sheikh Jarrah huko Baytul Muqaddas.

Mapema jana Jumanne, wanajeshi makatili wa Israel walivamia kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Jenin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuua shahidi vijana wawili wa Kipalestina kwa kuwapiga risasi za kivita. Habari nyingine iliyoripotiwa leo inasema, kijana mwingine wa Kipalestina ameuawa shahidi kutokana na majeraha aliyopata wakati aliposhambuliwa na Wazayuni huko Bayt al Lahm.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa tamko kuhusu jinai hizo za Wazayuni na kusema kuwa, lawama za madhara yoyote ya jinia hizo zinabebwa na wanajeshi vamizi wa Israel na kwamba kwa mara nyingine harakati hiyo ya Kiislamu inasisitiza kuwa, jinai za Wazayuni za kuwateka nyara na kuwaua Wapalestina zitazidi kulifanya taifa hilo lishikamane zaidi na muqawama.

Mapambano ya Wapalestina hayabagua, wake kwa waume, vijana kwa wazee, watoto kwa watu wazima

 

Katika taarifa yake hiyo, HAMAS imewataka wakazi wote wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan washiriki katika wimbi la kona zote la kupambana na adui Mzayuni. Imewataka washiriki vilivyo katika harakati za Siku ya Hasira na wajitokeze kwa wingi katika kuwaunga mkono mateka wa Kipalestina na matukufu ya taifa hilo.

Brigedi za Quds nazo zimesema kufuatia kuuliwa shahidi vijana hao wa Kipalestina kwamba, adui Mzayuni atambue kuwa, moto wa wanamapambano wa Palestina utawachoma na kuwateketeza wanajeshi wote Wazayuni na maficho yao.