Muungano vamizi wa Saudia waendelea kuua Waislamu wasio na hatia Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80926-muungano_vamizi_wa_saudia_waendelea_kuua_waislamu_wasio_na_hatia_yemen
Jinai za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinaendelea dhidi ya Waislamu wa Yemen wakati huu dunia ikielekeza jicho lake katika mgogoro wa Ukraine.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 02, 2022 03:51 UTC
  • Muungano vamizi wa Saudia waendelea kuua Waislamu wasio na hatia Yemen

Jinai za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinaendelea dhidi ya Waislamu wa Yemen wakati huu dunia ikielekeza jicho lake katika mgogoro wa Ukraine.

Tangu mwezi Machi 2015 hadi hivi sasa, Saudia kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, Imarati, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel inaendelea kufanya mauaji dhidi ya wananchi wa nchi ya Kiarabu na Kiislamu ya Yemen kwa mashambulizi ya kila namna ya angani, ardhini na baharini.

Hadi hivi sasa zaidi ya wananchi 15,000 wa Yemen wameshauawa, makumi ya maelefu ya wengine wameshajeruhiwa na mamilioni ya Wayemen wamekuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo.

Televisheni ya al Masirah imeripoti kuwa, maeneo mbalimbali ya mkoa wa Saada wa kaskazini mwa Yemen jana Jumanne yaliendelea kushambuliwa vikali kwa ndege na mizinga ya ukoo wa Aal Saud na wavamizi wenzake.

Saudia wanafanya jinai zisizo na kifani dhidi ya watoto na watu wasio na ulinzi huko Yemen

 

 

Kwa mujibu wa televisheni hiyo, aneo la Shada mkoani Saada ndilo lililolengwa zaidi na mashambulizi ya Wasaudia na kupelekea Waislamu wengi kujeruhiwa.

Hisham Sharaf Abdullah, Waziri wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen kabla ya hapo alikuwa amesema kwamba, wavamizi ambao wameshindwa kupigana vita katika medani za mapambano, wameamua kumalizia hamaki zao katika maeneo ya raia na kuua kwa umati watuuo wasio na hatia.

Mashambulio ya wavamizi wa Yemen dhidi ya makazi ya raia yameongezeka baada ya wanamapambano wa Yemen kuendelea kupata mafanikio na ushindi mkubwa katika medani za mapigano hasa kwenye mji wa Ma'rib.