Wazayuni wafurahishwa na matamshi ya Bin Salman
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81034-wazayuni_wafurahishwa_na_matamshi_ya_bin_salman
Matamshi ya Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia kuhusu utawala wa Kizayuni wa Israel yamewafurahishwa mno Wazayuni kiasi kwamba yameakisiwa kwa wingi na vyombo mbalimbali vya habari vya Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2022 04:02 UTC
  • Wazayuni wafurahishwa na matamshi ya Bin Salman

Matamshi ya Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia kuhusu utawala wa Kizayuni wa Israel yamewafurahishwa mno Wazayuni kiasi kwamba yameakisiwa kwa wingi na vyombo mbalimbali vya habari vya Israel.

Akihojiwa na jarida la Atlantic, mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia amesema, wao hawaihesabu Israel kuwa ni adui yao bali wanaihesabu kuwa ni mshirika wao kutaka na kukataa. Amedai kuwa kuna manufaa mengi ya pamoja baina yao na Wazayuni na kuna haja ya kushirikiana na utawala wa Kizayuni kufanikisha manufaa yao hayo. Amesema, kuna baadhi ya mambo inabidi yatafutiwe ufumbuzi kabla ya kufikia huko walikokukusudia wao na Wazayuni.

Edy Cohen, mwandishi wa habari Mzayuni ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba, kuanzia sasa, Msaudia yeyote atakayesema kuwa Wazayuni ni maadui zake, ajue kuwa anapingana na msimamo wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, Mohammad bin Salman.

Bendera ya utawala wa Kizayuni

 

Huko nyuma, Faisal bin Farhan, waziri wa mambo ya nje wa Saudia Arabia naye alikuwa amesema kuwa, kuingizwa na kukubaliwa utawala wa Kizayuni katika eneo hili si kwa manufaa ya Israel tu, lakini pia ni kwa manufaa na faida ya eneo hili zima.

Matamshi hayo ya viongozi wa Saudi Arabia yanatolewa katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel ni mtenda jinai mkubwa ambaye kila leo anamwaga damu za Waislamu hasa wa Palestina.

Utawala wa Kizayuni unazikalia kwa mabavu ardhi za nchi zote za Waislamu zilizoizunguka na ni utawala pandikizi ambao umeundwa baada ya kufanyika jinai kubwa mno dhidi ya Waislamu walioporwa ardhi zao na maeneo yao matakatifu kikiwemo Kibla cha Kwanza cha Waislamu ambacho hivi sasa kinakaliwa kwa mabavu na Wazayuni.