Iran na Imarati kushirikiana zaidi katika kukabiliana na uchafuzi wa vumbi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i85718-iran_na_imarati_kushirikiana_zaidi_katika_kukabiliana_na_uchafuzi_wa_vumbi
Msemaji wa Shirika la Kulinda Mazingira la Iran amesemam kuwa Tehran na Abu Dhabi zitaimarisha ushirikiano kati yao ili kukabiliana na msambao wa vumbi angani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 11, 2022 03:23 UTC
  • Iran na Imarati kushirikiana zaidi katika kukabiliana na uchafuzi wa vumbi

Msemaji wa Shirika la Kulinda Mazingira la Iran amesemam kuwa Tehran na Abu Dhabi zitaimarisha ushirikiano kati yao ili kukabiliana na msambao wa vumbi angani.

Kimbunga cha mchanga na vumbi ambacho ni natija ya awali ya ujenzi wa bwawa kubwa unaofanywa na Uturuki miezi kadhaa iliyopita kiliathiri anga za baadhi ya nchi na Iran kwa upande wa magharibi zikiwemo Syria, Iraq na Jordan.

Uturuki na mradi wa ujenzi wa bwawa kubwa

Ufuatiliaji wa ramani ya chembe ndogondogo za vumbi katika Tovuti ya Kimataifa ya Barcelona unaonyesha kuwa,  wimbi la vumbi hilo la karibuni awali liliathiri maeneo mengi ya Iraq na Syria na kisha kuingia Iran. Watu kadhaa wamepoteza maisha hadi sasa kutokana na kimbunga hicho cha mchanga na vumbi kilichoathiri baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq; huku maelfu ya wengine pia wakilazwa hospitali kwa matatizo ya kupumua. 

Hapa Iran pia baadhi ya miji imesitisha huduma kutokana na wimbi hilo tajwa la kimbunga cha mchanga na vumbi. Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Nourollah Moradi Msemaji wa Shirika la Kulinda Mazingira la Iran amesema, kesho Jumanne Iran na Imarati zitasaini hati za ushirikiano katika sekta ya mazingira ili kukabiliana na vimbunga vya mchanga na vumbi. Utaaji saini huo utahudhuriwa na Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Kulinda Maizngira la Iran na Waziri wa Imarati Anayehusika na Mabadiliko ya Tabianchi.