Katibu Mkuu wa Arab League: Iraq imefanikiwa kuzuia uchochezi
(last modified Wed, 07 Sep 2022 07:59:18 GMT )
Sep 07, 2022 07:59 UTC
  • Katibu Mkuu wa Arab League: Iraq imefanikiwa kuzuia uchochezi

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) ameashiria baadhi ya mapigano ya hivi karibuni katika kivuli cha mivutano ya kisiasa huko Iraq na mbinu za viongozi wa nchi hiyo kwa lengo la kuhitimisha hali hiyo na kueleza kuwa: Iraq imeweza kudhibiti uchochezi nchini.

Hali ya mambo ilichafuka huko Iraq wiki kadhaa zilizopota baada ya kujiri maandamano ya wafuasi wa harakati ya al  Sadr. Wafuasi hao Muqtada Sadr walizivamia taasisi mbalimbali za serikali baada ya kiongozi wa harakati hiyo ya Sayyid Muqtada Sadr kutangaza kujiengua katika uga wa kisiasa.Maandamano hayo hatimaye yalisababisha  mapigano kati ya kati yao na askari usalama. 

Muqtada Sadr

Muqtada Sadr baadaye aliwahutubia wananchi wa Iraq na kuwaomba radhi baada ya kupamba moto machafuko nchini humo. Sadr aidha alitoa muhula wa saa 24 akiwataka wafuasi wake kuondoka haraka katika eneo la ukanda wa kijani huko Baghdad; hatua iliyopelekea  hali ya mambo kurejea kama kawaida. 

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Ahmad Abu Ghait Katibu Mkuu wa Arab League amesema kuwa, Iraq imeweza kudhibiti uchochezi nchini ambao ulikaribia kuitumbukiza nchi hiyo katika mapigano na machafuko.

Abu Ghait ameyatolea wito makundi ya kisiasa ya Iraq kuyapatia ufumbuzi matatizo ya nchi hiyo ndani ya nchi. Vyama vya kisiasa nchini Iraq hadi sasa vimeshindwa kuunda serikali mpya baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mwezi Oktoba mwaka jana.