Jun 12, 2016 13:14 UTC
  • Wanazuoni Bahrain wapigwa marufuku kuendesha shughuli za kisiasa

Mfalme wa Bahrain ametoa dikrii ya kubadilishwa baadhi ya vipengee vya kisheria kuhusu vyama vya kisiasa.

Mfalme Hamad bin Issa Aal Khalifa ametoa dikrii ya kubadilishwa baadhi ya vipengee vya kisheria kuhusu vyama vya kisiasa na kupiga marufuku shughuli za siasa zinazoendeshwa na vituo vya kidini na wanazuoni nchini humo.

Kwa mujibu wa dikrii hiyo, ni marufuku huko Bahraini kutumiwa mimbari za kidini na hotuba kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kuwa na uhusiano na maafisa wa vituo vya kidini na vyama vya kisiasa.

Wakati huo huo vikosi vya usalama vya utawala wa Aal Khalifa hadi sasa vimewatia mbaroni maulamaa wengi kwa sababu tu ya kuzungumzia masuala ya kisiasa ma kijamii katika hotuba za Swala ya Ijumaa.

Bahrain imekuwa ikishuhudia maandamano ya amani ya raia wa nchi hiyo tangu mwaka 2011 dhidi ya utawala ulioko madarakani wa ukoo wa Aal Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa huru, kutendewa uadilifu, kukomeshwa vitendo vya kibaguzi na kuingia madarakani serikali halali ya kidemokrasia.

Tags