Jun 20, 2016 14:25 UTC
  • Bahrain yamnyang'anya uraia Ayatullah Issa Qasim

Utawala wa kizazi cha Aal Khalifa nchini Bahrain umeendeleza ukiukaji wake mkubwa wa haki za binadamu kwa kumnyang'anya uraia mwanazuoni mkubwa na mashuhuri wa Kiislamu nchini humo Ayatullah Issa Ahmad Qasim.

Uamuzi huo wa serikali ya Bahrain umelaani vikali na mashirika na jumuiya mbalimbali za Bahrain ambazo zimesema utawala wa Aal Khalifa umevuka mistari myekundu.

Harakati ya Waunga Mkono Mapinduzi ya Februari 14 ya Bahrain imesema utawala wa Aal Khalifa umedhihirisha tena sera zake za ubaguzi wa kimadhehebu na kikaumu kwa amri ya mabwana zake yaani Marekani, Uingereza na Saudi Arabia.

Serikali ya kifalme ya Bahrain imekuwa ikitekeleza siasa za ngumi ya chuma kukandamiza harakati ya wananchi wanaodai haki zao za kimsingi. Mamia ya wanaharakati wa masuala ya kijamii na kisiasa wameswekwa jela nchini humo kwa tuhuma zisizo na msingi na wengine wamekuwa wakinyang'anywa uraia ili kuzima midomo yao.

Tangu tarehe 14 Februari mwaka 2011 Wabahrain walianzisha harakati ya upinzani ya kudai uhuru, uadilifu, kukomeshwa ubaguzi na kukabidhiwa madaraka ya nchi kwa utwala wa kidemokrasia utakaochaguzi na wananchi.

Tags