Brigedi ya Jenin: Adui Mzayuni hatanusa harufu ya amani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i97048-brigedi_ya_jenin_adui_mzayuni_hatanusa_harufu_ya_amani
Brigedi ya Jenin yenye mfungamano na Saraya al-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa, utawala ghasibu wa Israel hautaona amani, na Wazayuni watajutia waliyoyafanya.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
May 06, 2023 03:15 UTC
  • Brigedi ya Jenin: Adui Mzayuni hatanusa harufu ya amani

Brigedi ya Jenin yenye mfungamano na Saraya al-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa, utawala ghasibu wa Israel hautaona amani, na Wazayuni watajutia waliyoyafanya.

Brigedi ya Jenin imetangaza katika taarifa yake wakati wa shughuli ya kuwakumbuka mashahidi watatu wa Kipalestina na shahidi "Sheikh Khizr Adnan" kwamba: Hatutanyamazia kimya haki yetu ya kujibu jinai ya mauaji ya "Khizr Adnan" na hatutatulia hadi tutakapotia majuto ndani ya moyo wa adui na kumfanya ajutie alichokifanya, na hatimaye kufurahisha nyoyo za watu wa Palestina.

Brigedi ya Jenin imesisitiza katika taarifa hiyo kuwa, makundi yote ya Saraya al-Quds katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan yatafuata nyayo za Sheikh Khizr Adnan na kuongeza: "Silaha zetu ni halali na jihadi yetu inaendelea katika nyanja zote. "

Katika siku chache zilizopita, makundi ya mapambano ya Palestina, yamekuwa yakitoa taaifa ya kusisitizia udharura wa kulipiza kisasi cha kuuawa shahidi Sheikh Khizr Adnan.

Shahidi Khizr Adnan aliyekuwa na umri wa miaka 44, mmoja wa viongozi wa harakati ya Jihad Islami na mfungwa wa muda mrefu wa Kipalestina katika jela za utawala wa Kizayuni, alikufa shahidi asubuhi ya Jumanne, Mei 2, 2023, baada ya siku 86 za mgomo wa kula akipinga kuzuiliwa kwa muda mrefu na utawala ghasibu na bila sababu yoyote.