-
Kwa nini Uhispania imeongeza mashinikizo dhidi ya Israel?
May 21, 2025 22:48Bunge la Uhispania limepitisha muswada unaoitaka serikali ya nchi hiyo kuacha kuuzia utawala ghasibu wa Israel zana zozote za kijeshi.
-
Wapalestina 26 wamekufa kwa njaa Ghaza katika muda wa saa 24 zilizopita
May 21, 2025 06:41Shirika moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema kuwa, takriban Wapalestina 26, wakiwemo watoto wadogo 9, wamekufa kutokana na njaa na ukosefu wa msaada wa matibabu katika Ukanda wa Ghaza unaozingirwa kila upande, kwenye kipindi cha saa 24 zilizopita.
-
Afisa wa Kizayuni: Israel inaua watoto wachanga kwa ajili ya burudani
May 21, 2025 04:00Mkuu wa Chama cha Democrats cha Israel amekosoa jinai za kivita za utawala wa Kizayuni na kusema: "Israel inaua watoto wachanga kwa ajili ya kujifurahisha, na mwenendo huu unaonyesha kutengwa na kukataliwa kwa utawala huo kimataifa."
-
Yemen yaiwekea mzingiro Bandari ya Haifa ili kuiunga mkono Palestina
May 20, 2025 22:56Yemen imetangaza habari ya kuifunga Bandari ya Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kupachikwa jina bandia la Israel, ili kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kujibu mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Ghadhabu za asasi za Marekani kutokana na kushadidi jinai za Israel Ukanda wa Gaza
May 20, 2025 22:55Sisitizo la utawala ghasibu wa Israel la kuendeleza vita vya kutisha vya Gaza katika mwezi wake wa ishirini na mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina, kuitumia njaa kama silaha na kuunda baa la njaa bandia huko Gaza kumepelekea kuibuka radiamali za kimataifa ikiwemo ndani ya Marekani.
-
Jinai za Israel ni kubwa mpaka UK, Canada na Ufaransa zatishia kuiwekea vikwazo
May 20, 2025 03:24Jinai za utawala wa Kizayuni ni kubwa mno na hazivumiliki kiasi kwamba hata viongozi wa Uingereza, Canada na Ufaransa wametishia kuiwekea vikwazo Israel kutokana na uhalifu wa kivita na jinai za kutisha huko Ghaza. Tishio hilo limezidisha mashinikizo kwa nduli wa Ghaza, yaani waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
-
Israel yaendeleza mashambulio ya kiwendawazimu Ghaza
May 20, 2025 03:24Duru za habari za ndani ya Palestina zimeripoti mapema leo Jumanne kwamba ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi makali na ya kiwendawazimu katika maeneo mbalimbali ya mji wa Ghaza.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq atoa wito wa utulivu na ushirikishwaji wa kisiasa Syria
May 20, 2025 02:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein, amesisitiza umuhimu wa utulivu, usalama, na mchakato wa kisiasa jumuishi nchini Syria, akieleza kuwa makundi yote na vikundi vya kijamii vinapaswa kushiriki katika kuunda mustakabali wa taifa hilo la Kiarabu.
-
Ahmadian: Iran na Pakistan hazitaruhusu usalama wa kikanda kutumiwa vibaya na maadui
May 20, 2025 02:53Afisa usalama wa ngazi ya juu wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan kamwe hazitaruhusu usalama wa kanda hii kutumiwa vibaya na maadui.
-
UNRWA yatahadharisha: Ukanda wa Gaza upo kwenye ukingo wa njaa
May 19, 2025 08:36Philippe Lazaarini Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa kuzingirwa eneo hilo na utawala wa Kizayuni kunakwamisha misaada ya kibinadamu kuingia katika hilo; kwa hiyo wakazi wa eneo hilo wapo kwenye ukingo wa njaa.