-
Hamas yasema hatua ya Israel kuzuia misaada kuingia Gaza ni ‘Uhalifu wa Kivita’
Mar 12, 2025 09:11Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema kuwa uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kuzuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu na mahitaji ya msingi katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa ni "uhalifu wa kivita."
-
Yemen yaanza tena kushambulia meli za Israel baada ya kukataa kufungua vivuko vya Ghaza
Mar 11, 2025 23:42Yemen imetangaza kuanza tena operesheni za kijeshi za kushambulia meli za Israel katika maeneo muhimu ya baharini karibu na fukwe zake kufuatia kumalizika muda wa mwisho ilioupa utawala wa Kizayuni wa kufungua tena vivuko vya Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada kuwafikia Wapalestina iliowasababishia hasara kubwa kutokana na mashamblizi yake ya kikatili ya zaidi ya miezi 15.
-
Duru za Palestina zakanusha madai ya US kwamba HAMAS imekubali kupokonywa silaha
Mar 11, 2025 23:10Duru moja ya Palestina yenye taarifa za mazungumzo yaliyofanyika kati ya HAMAS na serikali ya Marekani imekanusha ripoti zinazodai kuwa harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina imekubali kupokonywa silaha mkabala wa kutekelezwa usitishaji vita baina yake na utawala wa Kizayuni wa muda mrefu huko Gaza.
-
Jeshi la Kizayuni lavamia nyumba kwa nyumba Ukingo wa Magharibi, lawakamata Wapalestina 200
Mar 11, 2025 23:09Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limefanya uvamizi wa nyumba kwa nyumba katika mji wa Palestina wa Azzun, mashariki mwa Qalqilya kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika wimbi jipya la ushadidishaji hujuma na mashambulio katika eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu.
-
Wanawake wa Palestina wanalishwa futari zilizooza kwenye jela za Israel
Mar 11, 2025 08:05Mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa kidhulma katika jela za Israel ikiwemo ile jela ya Damon wanaishi katika mateso makubwa yasiyoelezeka hasa ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kula vyakula vilivyooza wakati wa futari na kutangaziwa nyakati sizo za wakati wa daku na futari.
-
Al Houthi: Tupo tayari kutekeleza oparesheni dhidi ya Israel iwapo haitaruhusu misaada kuingia Gaza
Mar 11, 2025 03:35Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amethibitisha msimamo wa harakati hiyo kuhusu muhula walioutoa kwa Israel ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
-
Hamas: Taifa la Palestina litajitawala lenyewe katika ardhi yake
Mar 11, 2025 03:32Mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema: "Gaza" na "Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni mali ya wenyeji wa maeneo hayo.
-
UN: Mashambulizi ya Israel yamepelekea Wapalestina 40,000 kupoteza makazi
Mar 11, 2025 01:02Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema kuwa uvamizi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi umesababisha "uhamishaji mkubwa wa watu" ambao haujawahi kushuhudiwa tangu vita vya mwaka 1967, vilivyosababisha kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Hizbullah: Muqawama uliilazimisha Israel kukubali usitishaji vita
Mar 10, 2025 07:56Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah amesema Israel ilikubali kusitisha mapigano na Lebanon baada ya kupata vipigo vikali kutoka kwa wapiganaji shupavu wa Muqawama.
-
Ansarullah: Matakfiri Syria ni vikaragosi vya madola ajinabi
Mar 10, 2025 07:55Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani vikali machafuko mabaya yaliyotokea hivi karibuni katika eneo la pwani ya magharibi mwa Syria na kusisitiza kuwa, mbali na kuwa ghasia hizo ni tishio kwa wahusika wa jinai hizo na walezi wao, lakini pia ni somo kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu.