-
Wapiganaji wa Muqawama Iraq washambulia kituo 'muhimu' cha kijeshi cha Israel
Mar 31, 2024 03:06Kundi la Wapiganaji wa Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) Iraq limetangaza kushambulia kituo "muhimu" cha kijeshi cha utawala wa Israel kilichoko kaskazini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu katika kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wanastahimili vita vya mauaji ya halaiki ya Israel.
-
Licha ya kuikosoa Israel hadharani, Biden ameidhinisha kwa siri silaha mpya za kuwaulia Wapalestina
Mar 30, 2024 22:48Rais Joe Biden wa Marekani hivi karibuni ameidhinisha kwa siri kupatiwa utawala wa Kizayuni wa Israel silaha mpya za kivita zenye gharama ya mabilioni ya dola zikiwemo aina za kisasa za mabomu na ndege za kivita.
-
61% ya Waisraeli hawaamini kama vita vya Ghaza vitamalizika kwa kusambaratishwa HAMAS
Mar 30, 2024 22:46Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa Palestina inayokaliwa kwa mabavu iliyopandikizwa jina bandia la Israel yanaonyesha kuwa asilimia 61 ya Wazayuni hawaamini kama vita vya Ghaza vitamalizika kwa "kusambaratishwa harakati ya Hamas".
-
Kwa mnasaba wa "Siku ya Ardhi", HAMAS yautolea wito Umma wa Kiislamu kuikomboa Palestina
Mar 30, 2024 22:45Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa taarifa maalumu kwa mnasaba wa "Siku ya Ardhi" ikisisitiza kuwa kuikomboa ardhi ya Palestina na matakatifu yake ni jukumu la Umma wote wa Kiislamu.
-
Saudia yaongoza katika kutupa chakula (israfu) duniani
Mar 30, 2024 07:58Saudi Arabia inaongoza kwa israfu au kutupa chakula duniani huku mamilioni ya watu wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula wakiwemo Wapalestina wa Gaza wanaokabiliwa na hujuma ya Israel.
-
Jeshi la Israel lakiri kuwaua na kuwazika Wapalestina wawili kwa tingatinga
Mar 30, 2024 02:34Televisheni ya CNN ya Marekani imenukuu taarifa ya jeshi la Israel likikiri kuwaua Wapalestina wawili na kufukia miili yao kwa kutumia tingatinga, baada ya televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kurusha hewani kipande cha video kinachoonyesha undani wa mauaji hayo.
-
Hizbullah yajibu mapigo, yashambulia vitongoji vya walowezi wa Kizayuni
Mar 29, 2024 22:58Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kambi kadhaa za Israel kaskazini mwa maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu mwaka 1948, kama sehemu ya awamu nyingine ya operesheni za kulipiza kisasi dhidi ya utawala huo na kuwatetea watu wa Gaza.
-
HAMAS: Misimamo ya Israel imekwamisha mazungumzo ya Doha
Mar 29, 2024 08:29Mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mazungumzo ya kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza yamegonga mwamba huko Doha, mji mkuu wa Qatar kutokana na misimamo isiyoeleweka ya utawala haramu wa Israel.
-
Watu 38 wauawa katika hujuma za anga za Israel Syria, Iran yalaani
Mar 29, 2024 08:28Kwa akali watu 38 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji wa Aleppo (Halab) huko kaskazini mwa Syria.
-
Wamorocco waungana na Wajordan kuzitaka serikali zao zivunje uhusiano na Israel
Mar 29, 2024 04:30Maelfu ya watu wameandamana katika nchi za Jordan na Morocco kuonyesha mshikamano na Wapalestina ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya kinyama vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa takriban miezi sita sasa, sambamba na kutoa wito kwa serikali zao wa kuvunja uhusiano na utawala huo ghasibu.