-
Watoto; wahanga wakuu wa vita vya miaka 8 nchini Yemen
Mar 27, 2023 03:50Mwaka wa 8 wa vita dhidi ya Yemen umemalizika huku takwimu zikionyesha kuwa, kwa wastani, mtoto mmoja wa Yemen anafariki dunia kila baada ya dakika 10 katika vita hivyo.
-
Kata'ib Hizbullah: Ikilazimu, tutakabiliana moja kwa moja na Marekani
Mar 26, 2023 22:41Harakati ya kupambana na ugaidi ya Kata'ib Hizbullah ya Iraq imeonya kuwa, iwapo makundi ya muqawama katika nchi hiyo ya Kiarabu yatashambuliwa na vikosi vya Marekani kama vilivyofanya Syria, basi harakati hiyo haitakuwa na budi kuingia katika makabiliano ya moja kwa moja na vikosi hivyo vamizi.
-
Jordan yalaani upanuzi wa vitongoji vya walowezi unaofanywa na Israel
Mar 26, 2023 22:41Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jordan imelaani hatua ya utawala haramu wa Israel ya kujenga nyumba nyingine mpya zaidi ya 8,000 ikiwa ni katika mpango wa upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huko Palestina.
-
Kundi la Iraq latangaza kuhusika na shambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Syria
Mar 26, 2023 07:58Kundi la Iraq linalojulikana kwa jina la Brigedi ya al Ghaliboun (Ghaliboun Brigade) limetangaza kuhusika na shambulio dhidi ya kambi ya wanajeshi vamizi wa Marekani iliyoko mashariki mwa Syria na kutoa onyo kwa wanajeshi hao.
-
Duru mpya ya oparesheni za kijeshi dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Syria
Mar 26, 2023 06:50Vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Syria vimelengwa kwa makombora, na Marekani nayo kutoa jibu kwa oparesheni hiyo kwa kutekeleza mashambulizi.
-
Askari wa Kizayuni wawashambulia Wapalestina waliokaa Itikafu kwenye Msikiti wa Al-Aqsa
Mar 26, 2023 04:30Askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel wamevamia Msikiti wa Al-Aqsa na kuwatia nguvuni Wapalestina kadhaa waliokuwa kwenye Itikafu na ibada zingine za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Hatua za Saudi Arabia na Qatar kwa ajili ya kurejesha uhusiano na Syria
Mar 25, 2023 09:56Nchi za Kiarabu zimeamua kurekebisha sera zao kuhusiana na Syria na sasa zimeweka mguu katika njia ya mazungumzo na kurejesha uhusiano na serikali ya Damascus.
-
Ripoti: Zaidi ya watu 18,000 wameuawa nchini Yemen kufuatia mashambulio ya Saudia na washirika wake
Mar 25, 2023 08:45Kituo cha Haki za Binadamu cha Ain kimetangaza kuwa, zaidi ya watu 18,000 wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma na mashambulio ya Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya nchi masikini ya Yemen.
-
HAMAS: Mapambano dhidi ya Israel yataendelea mpaka Aqsa ikombolewe
Mar 25, 2023 03:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mapambano yao kwa kushirikiana na makundi mengine ya muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yataendelea hadi pale Msikiti wa al-Aqsa utakapokombolewa.
-
Vikosi vamizi vya US vyashambuliwa kwa maroketi mashariki ya Syria
Mar 25, 2023 03:38Kambi mbili haramu za wanajeshi vamizi wa Marekani zimeshambuliwa kwa makumi ya maroketi huko mashariki mwa Syria.