Oct 22, 2023 03:21 UTC

Wakati wa ziara yake ya kutembelea msikiti mjini Toronto, Waziri Mkuu wa Canada amezomewa na hadhirina kotokana na msimamo wake kuhusu mauajii yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza huko Palestina ambako amepatwa na tahayuri asijue la kufanya.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, akikabiliana na umati wa watu waliokuwa wakimzomea, huku baadhi ya waliohudhuria msikitini wakitoa nara: "aibu juu yako". Waandamanaji hao Wamewataka waandaaji wa mkutano huo wasimruhusu Justin Trudeau kuzungumza.

Pia, wakati Trudeau anatoka kwenye jengo la msikiti, alikumbana na  waandamanaji waliokuwa na mabango yenye maandishi yanayowaunga mkono watu wa Palestina.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada ilitangaza baada ya tukio hilo kwamba: Trudeau alikuwa msikitini hapo kuhudhuria programu ya Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu ya Toronto ili eti kuonyesha uungaji mkono wake kwa jamii ya Waislamu ambao wameathiriwa na matukio ya kutisha katika Mashariki ya Kati. Waandamanaji waliokuwa eneo hilo wameitambua ziara hiyo ya Waziri Mkuu wa Canada eneo la msikiti wa Waislamu mjini Toronto kuwa ni unafiki na kukosa haya, hasa baada ya kutangaza uungano mkono wake kwa mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, kama viongozi wengine wengi wa nchi za Magharibi, amewakasirisha Waislamu wa Canada na maeneo mengine ya dunia kwa kusema kuwa, Ottawa inaunga mkono haki ya Israeli ya kujilinda, wakati huu ambapo utawala huo ghasibu ukiendelea kuua raia wasio na hatia wa Gaza. Waziri Mkuu wa Canada ametoa matamshi hayo huko Israel ikiwa tayari imeua raia zaidi ya elfu nne wa Gaza.

Mamia ya watoto wameuawa katika mashambulizi ya Israel, Gaza

Maandamano yanaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya dunia kupinga mauaji na mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya raia wa Palestina hususan katika Ukanda wa gaza, na vilevile kulaani uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa jinai na uhalifu unaofanwa na utawala wa kibaguzi wa Israel.