Uhispania, Ireland zaitaka EU kutazama upya uhusiano wake na Israel
(last modified Thu, 15 Feb 2024 07:41:41 GMT )
Feb 15, 2024 07:41 UTC
  • Pedro Sanchez
    Pedro Sanchez

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, amesema kuwa nchi yake na Ireland zimeiomba rasmi Kamisheni ya Ulaya kupitia upya uhusiano wake na Israel haraka iwezekanavyo. Sanchez amesema haya huku utawala wa Kizayuni wa Isarel ukiendeleza mashambulizi dhidi ya eneo la Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Uhispania ametuma ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X akiweka wazi hali mbaya inayolikabili eneo la Rafah kwa sasa na kuandika: Kuwajibika Umoja wa Ulaya kwa suala la  haki za binadamu na utu hakupasi kuwa na ubaguzi. 

Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Rafah 

Magazeti ya Times na El Pais ya Ireland na Uhispania kwa utaratibu yameripoti kuwa, wakuu wa nchi mbili hizo wamemtumia barua rasmi Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen.

Katika barua hiyo, viongozi wa Uhispania na Ireland wameihimiza Kamisheni ya Umoja wa Ulaya kufanya mapitio ya haraka ili kuona kama Israel inatekeleza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kupitia Mkataba wa Ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na utawala wa Israel ambao unaofanya  suala la kuheshimiwa haki za binadamu na kanuni za kidemokrasia kama kipengele muhimu cha uhusiano kati yao."

Pedro Sanchez na Leo Varadkar wamesema, wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya mambo ya Ukanda wa Gaza na kwamba kuendelea mashambulizi ya Israel katika maeneo mbalimbali ya Rafah ni tishio kubwa  ambalo jamii ya kimataifa inapaswa kukabiliana nalo bila kuchelewa."