Apr 13, 2024 12:08 UTC
  • RSF: Kulenga waandishi wa habari huko Gaza limekuwa jambo la

Shirika la Maripota Wasio na Mipaka (RSF) limelaani mashambulizi ya jeshi la Israel yaliyowalenga waandishi watatu wa habari jana, Ijumaa huko Gaza, na kusema kuwa kuwalenga waandishi wa habari limekuwa "jambo la kawaida sana."

Nii baada ya jeshi la Israel kuwajeruhi waandishi wa habari watatu katika shambulio la jana walipokuwa wakiripoti matukio ya kaskazini mwa kambi ya Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Jonathan Dagher, mkurugenzi wa ofisi ya Mashariki ya Kati wa shirika la Maripota Wasio na Mipaka, amesema kuwa shambulio hilo ni baya na halikubaliki.

Ameongeza kuwa zaidi ya waandishi wa habari 100 wameuawa na Israel huko Gaza katika kipindi cha miezi sita iliyopita, na amesisitiza haja ya kukomeshwa "mauaji," akitoa wito kwa jamii ya kimataifa "kuzidisha shinikizo" dhidi ya Israel.

Mashuhuda wa tukio hilo wameripoti kwamba, shambulio la mizinga la Israel lililenga kundi la waandishi wa habari, walipokuwa wakiripoti matukio ya kambi ya Nuseirat, ambayo inashuhudia operesheni ya kijeshi ya Israel.

Hii si mara ya kwanza kwa jeshi la Israel kushambulia waandishi wa habari katika mauaji ya kimbari yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza. 

Kwa mujibu wa data za Ofisi ya Vyombo vya Babari ya serikali huko Gaza, waandishi wa habari 140 wameuawa shahidi kutokana na mashambulizi ya Israel tangu tarehe saba ya Oktoba mwaka jana.