May 08, 2024 02:22 UTC
  • Utafiti: Wahamiaji nchini Ujerumani wanakabiliwa na umaskini kutokana na ubaguzi wa rangi

Utafiti mpya umebaini kuwa, wahamiaji nchini Ujerumani wanakabiliwa na hatari kubwa ya umaskini kutokana na ubaguzi wa rangi. Haya ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Utangamano na Utafiti wa Masuala ya Wahamiaji cha Ujerumani.

Wahamiaji hao wanaokumbana na vitendo vya ubaguzi wa rangi ni raia weusi, raia kutoka bara Asia na Waislamu. 

Utafiti huo umebaini kuwa kuna ongezeko la hatari ya umaskini linalohusishwa na aina nyingi za ubaguzi kama vile ubaguzi wa kimfumo, kitaasisi na mtu binafsi.

Raia weusi, raia kutoka nchi za Asia na Waislamu nchini Ujerumani wanakabiliwa na hatari kubwa ya umaskini kuliko Wajerumani wenyewe. Utafiti huo pia umegundua kuwa, ingawa karibu asilimia 10 ya Wajerumani walikurubia katika kiwango cha umaskini, lakini idadi kubwa zaidi ni raia weusi, watu kutoka bara Asia na wahamiaji Waislamu.

Ujerumani na ubaguzi 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, watu wenye rekodi ya kuhajiri mara nyingi wanakosa fursa za kufaidika pakubwa na taaluma zao, na pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali maeneo ya kazi kutokana na vitendo vya ubaguzi.

 

Tags