Moscow: Zelensky 'ana kichaa' kwa kutaka silaha za nyuklia za NATO
(last modified Thu, 06 Feb 2025 02:32:22 GMT )
Feb 06, 2025 02:32 UTC
  • Moscow: Zelensky 'ana kichaa' kwa kutaka silaha za nyuklia za NATO

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova amesema mwito wa Rais wa Ukraine, Vladimir Zelensky wa kutaka Kyev ipewe silaha za nyuklia na shirika la kijeshi la NATO unatia wasiwasi mkubwa.

Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii jana Jumatano, Zakharova alimtaja Zelensky kuwa "mwenda wazimu [aliyegubikwa na] njozi" na ambaye anaweza kutafuta 'bomu chafu'.

Katika mahojiano na mtangazaji wa televisheni ya Uingereza Piers Morgan siku ya Jumanne, Zelensky alikariri azma ya Kyev kumiliki silaha za nyuklia.

Ametoa wito kwa NATO kupeleka silaha za nyuklia nchini Ukraine kama hatua ya kukabiliana na Russia, wakati Kiev ikisubiri kujiunga na jumuiya hiyo ya kijeshi inayoongozwa na Marekani. “Je, tutapewa silaha za nyuklia? Basii watupe silaha za nyuklia,” Zelensky alimwambia Morgan.

"Ni makombora gani yanaweza kuzuia makombora ya nyuklia ya Russia? Amehoji Zelensy na kueleza kuwa, "Hilo ni swali la balagha?"

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova

Akijibu matamshi hayo ya Zelensky jana Jumatano, Zakharova aliandika: "Taarifa za hivi karibuni za Zelensky kwamba anataka kuwa na uwezo wa nyuklia zinamfichua kama chakaramu, ambaye anachukulia sayari kama kitu cha kupumbaza wake njozi zake za kiwendawazimu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kauli za Zelensy zinathibitisha kuwa, kwake, vituo vya nishati ya nyuklia sio chanzo cha nishati ya amani, lakini ni silaha chafu ambayo serikali ya Kyev inahitaji.