Jaribio la kwanza la kurusha roketi anga za juu barani Ulaya lafeli
(last modified Mon, 31 Mar 2025 11:40:08 GMT )
Mar 31, 2025 11:40 UTC
  • Jaribio la kwanza la kurusha roketi anga za juu barani Ulaya lafeli

Roketi la anga za juu la Ulaya limelipuka muda mfupi tu baada ya kuzinduliwa.

Katika ulimwengu wa kambi mbili wa kipindi cha Vita Baridi, Marekani na Umoja wa Kisovieti zilikuwa na ushindani mkubwa katika uwanja wa anga za mbali. Baada ya kuanguka Muungano wa Kisovieti mwaka wa 1991, Wazungu wa Ulaya walijikuta wakiitegemea sana Marekani katika teknolojiia ya anga za juu, na sasa wanafanya jitihada za kujitegemea katika sekta hiyo.

Ripoti zinasema, roketi la kwanza la anga ya Ulaya ambalo lilitakiwa kurushwa angani kwa kujitegemea kutoka barani humo limefeli na kushindwa kikamilifu.

Roketi la Spectrum, lililotengenezwa na kampuni ya Kijerumani ya Isar Aerospace, limerushwa kutoka kambi moja nchini Norway lakini limelipuka angani muda mfupi tu baada ya kuruka.

Roketi hilo limeshika moto muda mfupi baada ya kupaa kutoka Kituo cha Anga cha Andøya katika eneo la Arctic nchini Norway na kuanguka chini, suala lililosababisha mlipuko mkubwa.

Maafisa wa eneo hilo wanasema kuwa tukio hilo halikusababisha hasara yoyote au uharibifu ardhini.